IMEELEZWA kuwa,Mfuko wa Jimbo la Kigoma kusini umedaiwa kuwalipia wanafunzi hewa 22 ambao wameacha masomo katika shule mbalimbali katika wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma na kuingizia hasara serikali na jamii kiasi cha sh
.milioni 1,470,000.
Hayo yamebainika hivi karibuni katika kikao cha madiwani wilaya ya
Uvinza cha robo ya Nnne mwaka wa fedha ,ambapo mkaguzi wa ndani Jamwanga Adriano alibainisha changamoto hiyo inatokana na usimamizi mbovu wa kuibua watoto walengwa wa uhitaji wa mfuko
huo.
Alisema malengo yaliyokusudiwa na serikali haupo zaidi ya kuingizia hasara ya upotevu wa
fedha hizo,ambapo sheria ya `Fund Act
ya mwaka
2009 para ya 11(1)' ni kosa na
athari kwa watoto waishio katika mazingira magumu na kushauri ufuatiliaji wa fedha hizo sanjari na walengwa ili kuboresha wahitaji husika.
Adriano aliyataja majina walioacha masomo katika shule husika ni
pamoja na Pendo Matheo (mgaza),Kalialia Richard(nguruka),Said Alikula
(nguruka),Apensila Tama(nguruka) na wenzao 18 ambao wameacha shule na mmjoa
Leah Joram alikufa kwa ajali ya gari April,15,2014.
Diwan wa kata ya Ilagala
Hamis Mkwafi na kata ya
nguruka Abdallah Masanga kwa nyakati tofauti walipohojiwa na
gazeti hili wanafahamu kisa cha wanafunzi hao kutoweka
katika shule w alisema, hawajui na
kukiri walioacha wanatoka katika kata zao na kudai ugumu wa maisha unachangia
katika hilo.
“ukata wa kipato katika kaya
inachangia walengwa kuacha masomo,kutokana na mfuko kulipia ada tu,ili hali
michango mingine inamtaka mlezi atoe, hii inafifisha jitihada za serikali
husika” walianisha madiwani hao.
Walipohijiwa wanafahamu fedha zilizolipwa kwa wanafunzi 22
zipo wapi walisema kupitia taarifa ya mkaguzi wa ndani ,wameagiza kamati ya afya,elimu na maji wahakikishe kikao
kijacho kitakachofanyika Octoba mwaka huu wawe n a majibu sahihi na kuanisha watoto na fedha zilipo.
Kwa upande wa Ofisa
wa wanasheria wa kujitegemea Mkoa huo
Hamis Ramadhan alipoulizwa na Jamboleo changamoto hii kisheria
lipoje,alisema kwa mujibu wa sheria lipo katika makosa ya jinai wa wizi wa kuaminiwa kwa
mtoa fedha na mpokeaji.
Alibainisha kuwa kwa mtoaji fedha katika kifungu cha
301,302 hadi 305 inamtuhumu mtoaji
kufuja fedha za serikali na kuathiri mfumo kwa walengwa kwa kitendo cha kulipa ada kwa wanafunzi
hewa,ambapo akithibitika hivyo atahukumiwa jela miaka 7 na faini au vyote kwa
pamoja.
KAPIPIJhabari.COM ilipompigia simu ya
kiganjani jana mwenyekiti wa mfuko huo David Kafulila juu ya
hilo hakuwa hewani sanjari na mkurugenzi pamoja na ofisa elimu alipoulizwa hilo
walidai wana kikao.
No comments:
Post a Comment