Pages

KAPIPI TV

Sunday, August 3, 2014

INASIKITISHA SANA,...KIJANA ANAOMBA MSAADA WA MATIBABU YA MGONGO, WASILIANA NA MAMA YAKE MZAZI 0753 260 543 AU 0716 502 729-TABORA

Kijana Abdallah Ulemo(20)ambaye alipata ajali ya kuanguka juu  mnazi na kuvunjika baadhi ya mifupa ya mgongo amekuwa akifanyiwa msaada wa kutolewa nje kwakuwa hana uwezo wa kutembea wala kuukaa,mama yake mzazi amekuwa akilazimika kuomba msaada kwa majirani ili aweze kumbeba kumtoa nje na wakati mwingine hata huduma za usafi wa mwili,Kijana huyu ambaye alianguka tangu tarehe 29/Oktoba/2013 pamoja na juhudi za kumtafutia huduma za matibabu lakini kwasasa amekwama kuendelea na matibabu baada ya kukosa fedha ambapo inahitajika kiasi cha shilingi milioni 2 na nusu ili apelekwe hospitali ya rufaa ya Muhimbili jijini Dar-es-salaam,Kwa yeyote atakayeguswa anaweza kuwasiliana na mama yake mzazi ambaye ndiye anayemtunza kwasasa huku hali ya maisha ikiwa mbaya zaidi-WASILIANANAE KWA NAMBA 0753 260 543 AU 0716 502 729.
Abdallah akkiwa na mama yake mzazi wakati akizungumza na KAPIPIJhabari.COM kuhusu matatizo yanayomkabili ambapo kubwa zaidi anahitaji msaada wa matibabu licha ya kuwa ana matatizo ya kipato tangu mwaka 2013 alipopata ajali hiyo ambapo kwasasa mama yake mzazi analazimika kuacha shughuli nyingine ili aweze kumpa matunzo.Abdallah anaishi nyumbani kwa mama yake mzazi kata ya Gongoni manispaa ya Tabora mtaa wa Railway na Migazi.
Abdallah amekuwa akiomba msaada kwa ndugu na jamaa lakini bado hajafanikiwa kupata kiasi hicho cha fedha kinachohitajika na ameteseka kwa muda mrefu,"Jamani watanzania wenzangu naomba mnisaidie nateseka sana nilianguka kwenye mnazi hapa hapa nyumbani,nawaombeni sana kwa yeyote atakayeguswa na tatizo langu awasiliane na mama yangu mzazi  kwa simu hizo"Abdallah amekuwa akilia usiku na mchana na asijue nini la kufanya kwa hali aliyonayo.Ndoto zake za maisha zimepotea,akijiringanisha na vijana wenzake hasa marafiki wa karibu ambao wamekuwa wakijitafutia riziki na hata kuwasaidia wazazi wao lakini kwake imekuwa ni kinyume chake,amekuwa anasaidiwa na mama yake mzazi kama wakati alipokuwa amezaliwa na kuwa mtoto mchanga,hali hii imemsikitisha sana na kujikuta anabubujikwa na machozi kila kukicha.  



No comments: