Pages

KAPIPI TV

Sunday, July 27, 2014

TANZANIA YAPOKEA TUZO YA USAFIRI WA ANGA DUNIANI

20140704_114713
Tanzania imekuwa moja ya nchi nne Afrika iliyotunukiwa tuzo ya kimataifa ya usafiri wa anga duniani na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga duniani (ICAO) kutokana na mchango wake mkubwa katika ukuaji na usalama wa anga katika bara la Afrika.
Tuzo hiyo ilitolewa hivi karibuni mjini Dakar, Senegal na Rais wa ICAO, Dk. Bernard Aliu katika kikao cha 24 cha Kamisheni ya usafiri wa anga afrika.
Pichani Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, John Chacha akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Rais wa ICAO, Dk. Aliu

No comments: