SAKATA la
kutaka kuifuta Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye ulingo wa
siasa Kigoma limezidi kuchukua sura mpya,ambapo imebainika kiasi cha sh.milioni
10 kutumika katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Octoba 2014.
Wakati hali
ya siasa mkoani hapa kuwa tete baada ya viongozi 99 kukihujumu chama cha
chadema kwa kukimarisha chama kipya cha Alliance Transparecy For Change
Tanzania ,baadhi ya wanachama wa chadema wameuambia mtandao huu kuwa
aliyekuwa mwenyekiti Jaffari Kasisiko ni
muuaji wa demokrasia katika chama hicho.
Pamoja na
kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti huyo sambamba na kutumiwa na Mbunge wa Jimbo
la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kushawishi baadhi ya viongozi wakuu wa kila
sekta kujiunga na chama cha ACT.
Kutokana na
hali hiyo chadema imebaini Mbunge huyo
katika moja ya vikao vya chama cha ACT ambacho kilifanyika katika nyumba ya
aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Kasisiko kuwa atagharamia kampeni za
uchaguzi huo kwa lengo la kuweka mizizi ya chama kuanzia ngazi ya kijiji hadi
mkoa.
Mjumbe wa
Baraza la uongozi Chadema kanda ya
kati Alphonce Mbasa alisema wananchi wanafahamu
mbunge huyo ni sumu katika vyama
vya upinzani,kutokana na ukaidi wake ndani ya chadema sanjari na kukataa kujibu
tuhuma 11 za msingi juu ya kukihujumu chama,badala yake anashawishi umma kuwa
alionewa.
“ wazee wa
kigoma baadhi yao wanajua kila kitu na alionekana katika kikao hicho na kuahidi kutoa
fedha hizo pamoja na kujinadi rasmi siku ya uzinduzi wa ACT 1,septemba,2014 Mwanza , wananchi wa hapa ni
bendera ,baada ya miezi sita mtashuhudia siasa haina adui wala shosti”
aliainisha Mbasa.
Alisema kwa
aliyekuwa mwenyekiti chadema Jafar Kasisiko ni chachu ya kuua demokrasia ndani
ya chadema kwa kuwa alihodhi nyadhifa za ukaimu wa baraza la wazee na mwenyekiti wa mkoa kwa miaka 20,ambapo
katiba inasema kila baada ya miaka 5 kunakuwa na uchaguzi wa nafasi hiyo lakini
kimkoa hakufanya hivyo .
Alisema,
Chadema ipo mbioni kufanya uchaguzi wa viongozi upya katika sekta ya Bavicha,Bawacha na Bazecha kwa
kuchuja makapi ya chama cha ACT kwa dhati ya kujipanga kwenye shughuli zote za utendaji katika
uchaguzi wa serikali za mitaa sambamba na wabunge 2015.
KAPIPIJhabari.COM imebaini kuanzia Julai 27 hadi 31 chadema watakuwa na mchakato
wa kusimika viongozi katika idara nyeti sambamba na 2,Agosti ,2014 viongozi wa
juu wa chama hicho akiwemo Freeman Mbowe
watakuwa na kibarua cha kuzuru mikoa ya Katavi na Kigoma juu ya mustakabali
wa chama kwa umma.
Waratibu wa ACT mkoani Kigoma Sendwe Ibrahim na Juma Ramadhan walipohojiwa juu ya 14, Juni,
2014 ,saa 10 alasiri Zitto Kabwe akiwa
nyumbani kwa aliyekuwa mwenyekiti wa chadema kasisiko na wajumbe 22 wa chama cha ACT na kutoa ahadi hiyo akiwemo Meya wa manispaa ya
kigoma ujiji walisema si kweli na walipoulizwa ukweli hawakuwa tayari kutoa majibu sahihi.
Angalizo kwa
wananchi kwa ujumla wasome alama za
nyakati kwa kujitambua, kutafakari jambo
kwa umakini ili kufanya maamuzi bora bila kushinikizwa kabla ya kujiunga na chama husika,wahenga walinena
miluzi mingi humpoteza mbwa.
No comments:
Post a Comment