Pages

KAPIPI TV

Sunday, July 27, 2014

WANANCHI WA UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA WALIA NA JK

 
Na Magreth Magosso,Kigoma

WANANCHI wa vijiji vya ukanda wa Ziwa Tanganyika mkoa wa Kigoma,wataka ahadi ya ujenzi wa Barabara ya Chankele,Mwamgongo na  Kagunga iliyotolewa na Rais  Jakaya Kikwete itimizwe, ili waondokane  na  adha ya kutozwa  kodi  wa bidhaa  za  madukani kila watumiapo  usafiri wa maboti .
 
Kutokana na dhati na juhudi za rais huyo  kutaka kufufua na kuboresha miundombinu  ya vyombo vya usafiri katika mikoa iliyopo pembezoni mwa nchi,ambayo  zaidi ya miaka 50 ya uhuru hazina huduma bora za barabara,nishati na mitandao ya maji safi .
 
Changamoto hizo ni pamoja na mkoa wa kigoma hasa vijiji vya ukanda wa ziwa hilo,ambapo wakazi wake ni wahanga wa  kukosa usafiri wa maboti  yenye kukidhi viwango  bora vya usafiri huo, kutokana na kutopatiwa tiketi ,laifu jaketi  kwa tija ya  kufidiwa  pale janga  linapotokea  ziwani .
 
Wakizungumzia hilo katika kikao cha madiwani juzi kigoma ujiji, Baadhi ya madiwani Mathias Bwami na Habibu Hebeye walisema adha hiyo inachangiwa na halmashauri husika kushindwa kuwajibika katika maeneo lengwa ya kutoza ushuru hatimaye kutoza wananchi hao wasio na hatia .
 
Diwani wa Kata ya Mwamgongo Kassim Nyamkunga  na Hamis Betese  kata ya Mkigo walisema  Waziri Mizengo Pinda aliahidi kutoa milioni 300 katika mradi huo huku Katibu wa wizara ya Tamisemi akiwatupia lawama wataalamu wa halmashauri husika kwa kushindwa kuingiza katika  mchakato wa Bajeti za kitaifa.
 
Akichangia hilo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya Ramadhan Maneno Katibu tawala wa wilaya hiyo Elisha Joshua alisikitishwa na kitendo cha wananchi kutozwa kodi kwa bidhaa za madukani kisa kutumia usafiri wa boti ili hali wanajua tayari kodi walishalipia katika maduka husika.
 
Agiza   katika kikao cha kamati husika wahakikishe adha hiyo iwe moja ya ajenda Huku mwenyekiti wa halmashauri hiyo Betese akidai  wanakijiji  wa ziwani wanaishi katika maeneo hatarishi kiusafiri na kusisitiza mradi wa barabara hiyo itaondoa urasimu kwa watumishi wa idara husika kwa kutoza kodi marambili .
 
Aidha kero hiyo ni ya muda mrefu,ambapo baraza la madiwani walipeka katika kikao cha Rcc Mkoa ili kulipatia ufumbuzi lakini wananchi bado watozwa hadi leo,baadhi ya madiwani wa vijiji husika akiwemo Kassim Nyakunga anayetaka ahadi ya rais na waziri mkuu itimie kuondoa adha hiyo.

No comments: