Mkurugenzi wa Benki ya Posta Bw. Sabasaba Moshingi na Mkurugenzi Mkuu PSPF Adam Mayingu kulia wakifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma ya Wastaafu Loan mkopo unaotolewa na shirika hilo kwa kushirikiana na Benki ya Posta kwa wastaafu, Kulia wanaoshuhudia ni Katibu Mkuu Mstaafu Ndugu Philemon Luhanjo na kushoto ni Muuguzi Mstaafu na RAS wa mkoa wa Kilimanjaro Mama Eunice Temu, Uzinduzi huo umefanyika kwenye Jengo la PSPF lililopo Posta jijini Dar es salaam . Kutoka kulia ni Muuguzi Mstaafu na RAS wa mkoa wa Kilimanjaro Mama Eunice Temu, Mkurugenzi Mkuu PSPF Adam Mayingu, Katibu Mkuu Mstaafu Ndugu Philemon Luhanjo na Mkurugenzi wa Benki ya Posta Bw. Sabasaba Moshingi wakinyanyua mikono juu kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma hiyo. Katibu Mkuu Mstaafu Ndugu Philemon Luhanjo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wastaafu wanaopata huduma ya Wastaafu Loan. Katibu Mkuu Mstaafu Ndugu Philemon Luhanjo akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa vitengo wa mashirika hayo. Katibu Mkuu Mstaafu Ndugu Philemon Luhanjo katika picha ya pamoja na mameneja Katibu Mkuu Mstaafu Ndugu Philemon Luhanjo maofisa mbalimbali wa mashirika hayo. Katibu Mkuu Mstaafu Ndugu Philemon Luhanjo akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSPF Bw. Adam Mayingu akizungumza na wageni waalikwa. Mkurugenzi wa Benki ya Posta Bw. Sabasaba Moshingi akitoa hotuba yake katika uzinduzi huo. Msanii Mrisho Mpoto akifanya vitu vyake katika uzinduzi huo. Wasanii wa Bendi ya Mjomba Band wakiigiza igizo la wastaafu wanavyohangaika katika mifuko mbalimbali ya Pensheni Maofisa mbalimbali wa mashirika hayo wakiwa katika uzinduzi huo. Maofisa mbalimbali wa mashirika hayo wakiwa katika uzinduzi huo.
…………………………………………………………………….
Leo Juni 20, 2014 Mfuko wa
Pensheni wa PSPF kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania wamezindua
mpango maalum wa kutoa mikopo kwa wastaafu ambao unajuliakana kama
Wastaafu Loan, ambapo sasa wastaafu wa PSPF wanaweza kunufaika na mikopo
hiyo.
Lengo la mkopo huu ni kuwawezesha wastaafu kukidhi mahitaji
halisi ya fedha, na hatimaye kuboresha maisha yao. Miongoni mwa mahitaji
makubwa ya fedha kwa wastaafu ni pamoja na gharama za matibabu, ada za
shule, kuendesha biashara na miradi mbalimbali.
kwa muda mrefu sasa hapa nchini taasisi mbalimbali za fedha
zimekuwa hazitoi mikopo mbalimbali kwa wastaafu wakidhani kwamba
wastaafu hawana uwezo wa kulipa, na kujenga dhana ya kutokopesheka, kwa
kuliona hilo na kwa kutambua mchango wa wastaafu kwa taifa hili. PSPF
kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania tumebuni mpango huu wa
kipekee nchini wa kuwakopesha wastaafu wa Mfuko wa PSPF.
Katika utafiti tuliofanya umeonesha kuwa wastaafu kwa ujumla
wanaingiza kiasi kikubwa sana cha fedha katika uchumi kutokana na mafao
wanayolipwa. Mafao hayo yanaweza kuleta athari chanya (multiplier
effect) katika nyanja mbalimbali za kiuchumi kama vile kuongeza uwezo wa
kifedha katika taasisi za kifedha, kuongeza ajira, kukuza kipato,
kupunguza umaskini na kudumisha utulivu wa kisiasa nchini.
Hili
linawezekana iwapo fedha hizo zitatumika kwa busara na kuwekezwa katika
maeneo salama. Ni wajibu wa PSPF kutimiza dhana ya kuwakinga wastaafu na
majanga yote ya kiuchumi na ya kijamii yanayotokana na kupungukiwa na
kipato. Kwa kuzingatia hili Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa kushirikiana
na Benki ya Posta Tanzania umebuni na kuanzisha Mpango huu wa Mikopo kwa
Wastaafu wa Mfuko wa PSPF.
Hivyo tunapenda kuzishawishi taasisi za fedha ikiwemo mabenki na
wataalam wa uwekezaji na fedha kubuni njia mbalimbali za kuwasaidia
wastaafu ili waweze kuwekeza na kuendelea kufurahia maisha ya ustaafu.
Pia wataalam hao waangalie namna kuweka mipango ya kusaidia wastaafu
hapa nchini ambao kwa ujumla wao wana kiasi kikubwa cha fedha ambacho
kikitumiwa vyema kinaweza kuleta mchago mkubwa katika uchumi wa nchi.
Mpaka sasa zaidi ya wastaafu zaidi ya 2000 wamenufaika na mpango huu
ambao umeanza miezi mitatu iliyopita.
Mstaafu anayetaka kukopa hatahitaji kuwa na dhamana , pia mkopo
huu una bima, hivyo endapo mkopaji atafariki familia yake haitaendelea
kudaiwa, aidha, riba inayotozwa kwa mkopo huu ni ndogo ukilinganisha
na mikopo mingine, yaani asilimia 12 tu kwa mwaka. Wastaafu wote wa
mfuko wa PSPF wanaweza kupata mikopo hii ambayo marejesho yake ni kati
ya mwaka moja hadi miaka mitatu.
Ili kukopa unahitajika kwenda kwenye tawi lolote la Benki ya Postalililopo karibu yako
No comments:
Post a Comment