Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (MB) akikagua Gadi ya
Wanawake inayoundwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza katika
Maadhimisho ya Magereza Day yaliyofanyika leo Juni 20, 2014 katika
Viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam. Gadi
ya Wanaume iliyoundwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza
wakipita mbele ya Mgeni rasmi katika mwendo wa haraka wakati wa kutoa
heshima katika Maadhimisho ya Magereza Day yaliyofanyika katika Viwanja
vya Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga kilichopo Jijini Dar es Salaam. Msanii
Nguza Viking anayetumikia Kifungo chake Gerezani akiwa na Bendi ya
Wafungwa(anayepiga gitaa) akiimba Wimbo Maalum kuhusu Urekebishaji wa
Wafungwa unavyofanyika Magerezani(wa pili kulia) ni Jonson Nguza Maarufu
kwa jina la Papii Kocha wakitumbuiza katika Maadhimisho ya Magereza Day
yaliyofanyika leo Juni 20, 2014 katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa
Magereza Ukonga. Baadhi
ya Maafisa wa Jeshi la Magereza Nchini wakitoa heshima ya Utii wakati
Kikosi cha Bendera kikipita mbele ya Mgeni rasmi(hayupo pichani) katika
Maadhimisho ya Siku ya Magereza(Magereza Day) yaliyofanyika leo Juni 20,
2014 katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es
Salaam. Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja(aliyesimama)
akitoa maelezo mafupi kuhusu Madhumuni ya Maadhimisho ya Siku ya
Magereza(Magereza Day). Maadhimisho haya ya siku ya Magereza yanafanyika
hapa nchini kwa mara ya pili ambapo leo yamefanyika katika Chuo cha
Maafisa wa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam(wa Nne kulia katika
vazi la suti nyeusi) ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias
Chikawe(wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia,
Raphael Tuhaferi. Mkuu
wa Kitengo cha Kilimo na Mifugo Ndani ya Jeshi la Magereza, Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasan Kimaro(wa pili kushoto) akitoa
maelezo mafupi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias
Chikawe (suti nyeusi) kuhusu uzalishaji wa mafuta ya mawese ambayo
hutumika kwa matumizi ya Wafungwa Magerezani alipotembelea Banda la
Kilimo na Mifugo (wa pili kulia kwa Waziri) ni Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja. Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(MB) akipokea Salaam ya
heshima toka kwa Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maafisa wa Jeshi la
Magereza(hawapo pichani) katika maadhimisho ya Siku ya Magereza(Magereza
Day). Kushoto katika picha ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza,
John Casmir Minja (kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Maafisa wa Magereza
Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Erasmus Kundy.
No comments:
Post a Comment