Na Magreth Magosso,
Arusha
KAIMU
mkurugenzi Mkuu wa shirika la Hifadhi la
Taifa(TANAPA),Witness Shoo ametoa wito kwa wandishi wa habari nchini wathubutu kuelimisha jamii juu ya madhara ya
ujangili kwa wanyamapori sanjari na athari zake kwa lengo la kulinda aina za
wanyama waishio katika hifadhi husika kwa vizazi vijavyo siku za usoni.
Akitoa kauli
hiyo jijini Arusha katika ofisi kuu ya Mamlaka hiyo Witness Shoo alisema hivi
sasa
hifadhi ya Arusha haina mnyama aina ya Faru kutokana na ujangili
uliokithiri
miaka ya nyuma ,huku akihofu kutoweka kwa jamii ya wanyama aina ya Tembo kutokana na mauaji holela yanayoendelea katika hifadhi hiyo.
“Namini karne nne zijazo Taifa litabaki mufilisi kwa ujio wa watalii
kutoka nchi za Ughaibuni kutokana na kutoweka kwa wanyama adimu na changamoto ya mauaji ya Tembo yanayoshamiri
kila kukicha katika hifadhi za wanyama,jamii ibadilike wandishi tusaidiane katika
hili” alibainisha Shoo.
Msemaji wa
Shirika la hifadhi Tanapa Paschal Shelutete alisema
lengo la kuwashirikisha wandishi
wa habari katika shughuli zao ni moja ya jitihada kubwa kulenga shabaha ya
umma kupata usahihi wa kubaini changamoto za hifadhi sanjari kuelimisha jamii
zinazoishi karibu na hifadhi ziwajibike kulinda maliasili ya nchi ili vizazi
vyote vinufaike na urithi wa rasilimali za Taifa.
Naye Mkuu wa
Idara ya ujirani mwema Pendaeli Shafuri alisema jamii zinazoishi karibu na
hifadhi za Taifa hazina budi kutii sheria za misitu na wanyamapori kwa mujibu wa
sheria ili kuepusha misuguano isiyo na tija kwa leo na kesho,huku akikiri
ongezeko la jamii hizo ni chachu ya mgongano wa kuibiana mipaka na kudai
chnagamoto hiyo inafanyiwa kazi kwa lengo la kuboresha mahusiano na vijiji .
Ofisa Utalii
wa hifadhi hiyo Samweli Sakinoi akiri katika hifadhi za kaskazini zinakabiliwa
na vitendo vya ujangili,ambapo hivi sasa
hifadhi ya Arusha inakabiliwa na ukosefu wa mnyama aina ya Faru,kutokana
na jamii kutothamini,kuenzi uwepo wao,hali inayozorotesha shirikia kushindwa
kufikia malengo yake kiuchumi hasa uboreshaji huduma za kijamii kwa vijiji
jirani.
No comments:
Post a Comment