TATIZO la ongezoko la mimba kwa wanafunzi wa shule ya
sekondari Magala iliyopo kata ya Magala wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara
limepungua kwa kasi baada ya wanafunzi hao kupata msaada wa ujenzi wa bweni la
wasichana.
Akizungumzia hilo Matroni wa shule hiyo Stella Ezekieli
alisema baada kupata ufadhili wa ujenzi wa bweni la wasichana kutoka mamlaka ya
hifadhi ya manyara changamoto ya
wanafunzi kupata mimba imetoweka katika shule hiyo ambapo awali ilikuwa ni
tatizo kubwa kwa wanafunzi wa shule kupata mimba na kufukuzwa shule.
Alisema kuwa kipindi cha awali kila mwaka walikuwa
wanawafukuza wanafunzi zaidi ya sita kutokana na kuwa na mimba wakati wakiwa
shule jambo ambalo ni kosa kisheria mwanafunzi kuwa na mimba wakati akiwa
shule.
“Wanafunzi wa kata hii wanapanga katika majumba ya watu na
wengine wanatoka mbali hadi kufika shule tatizo hili limechangia kwa kiwango
kikubwa cha wanafunzi kupata mimba, ambapo tangu wanafunzi walipoanza kuishi
katika mabweni tatizo hilo halipo kabisa” alisema mwalimu Stella.
Alisema bweni hilo linauwezo wa kuchukua wanafunzi 80 ambapo
kwa sasa wapo 64 ambapo kipaumbele kimetolewa kwa wale wanaoishi maeneo ya
mbali na shule lengo ni usalama mzuri wasichana na wanatimiza malengo yao.
Aidha aliomba pia mabweni ya watoto wa kiume yaweze kujengwa ili nao wawe katika usalama wa
maisha yao wakati wa kuja shule ambapo eneo kubwa limezungukwa na msitu wa
hifadhi na kunawanyama wengi wenye madhara kama simba.
Wakitoa shukurani zao wanafunzi hao Ruth Paulo na Osiana
Thadei walisema ufadhili huo wa bweni imesaidia kupunguza adha walizokuwa
wanazipata wakati wa kufika shule kwa kuhofia wanyama wakali pamoja na kujaa
kwa mto magala kuwa chanzo cha wao kutozingatia taratibu za kufika shule kila
siku.
“Tangu kuanza kwa bweni hata masomo yamekuwa mepesi kwa kuwa
tunapata ushirikiano na walimu kutuelekeza pale ambapo hatujaelewa vizuri
lakini pia tatizo la mimba nalo limekwisha kwa wanafunzi na kuomba msaada huo
uendelee kwa ujenzi wa mabweni ya wavulana nao” walisema wanafunzi hao.
Aidha mhifadhi wa ujirani mwema hifadhi ya Manyara Ibrahimu
Minga alisema lengo la kujenga bweni hilo ni kuweka usalama wa wasichana ambapo
ujenzi huo ulifuatia maombi ya wakazi wa eneo hilo katika vipaumbele vyao vya
kijiji.
Alisema ujenzi huo umegharimu zaidi ya milioni 116 ambapo
wananchi walishiriki kuchangia nguvu zao ili jamii inufaike na maendeleo
yatokanayo na mapato ya utalii wa n je na ndani.
No comments:
Post a Comment