Mwanasiasa Mkongwe Mzee Kingunge Ngombale- Mwiru akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kutoka katika
mkutano wa pamoja kati yake na Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa
China, Mhe. Li Yuanchao(kulia) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama
cha Kikomunisti nchini China na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM) wa Tanzania Bara Philip Mangula, uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dares Salaam.
Picha zote na Magreth Kinabo -Maelezo
………………………………………………………………
Na Magreth Kinabo- Maelezo
Mwanasiasa Mkongwe nchini, Mzee
Kingunge Ngombale- Mwiru, ametoa changamoto kwa Watanzania kuwa wao
ndio watakaojenga misingi ya maendeleo ya Ujamaa na Kujitegemea.
Kauli hiyo ilitolewa leo na
Mzee Ngombale- Mwiru,mara baada ya kutoka katika mkutano wa pamoja
kati ya Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao,
ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Kikomunisti nchini China na
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wa Tanzania Bara Philip
Mangula, uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dares Salaam.
Mkutano huo ambao ulikuwa
ikijadili suala ya la ujenzi wa maendeleo ya Ujamaa na Kujitegemea ya
jamii ya Watanzania ulioanzishwa na waasisi wa ujamaa huo,ambao ni
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Mao Tse-tung .
“Lazima uendelee mchakato wa
ujamaa na kujitegemea. Kazi ya kujenga usawa ni ya kila mtu, watu
hawajengewi ujamaa wanajenga wenyewe”, alisema huku akisisitiza kwamba
wanatakiwa kushirikiana katika suala hilo.
Aliongeza kuwa ikiwa Watanzania watapuuza hakuna mtu anyaeweza kuwajengea maendeleo ya ujamaa huo.
Mzee Ngombale- Mwiru aliongeza
kwamba Watanzania wanapaswa kujenga uchumi wa kisasa wa kujitegemea
mfano vile kwa kubadilisha kilimo, ufugaji na uvuvi kuwa wa kisasa.
Aliwaasa vijana kuwa chachu ya mabadiliko hayo.
Kwa uapnde wake Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wa Tanzania Bara Philip Mangula,
alisema mkutano huo ulikuwa unazungumzia ujenzi wa ujamaa na maendeleo
ya kujitegemea, uchambuzi wa tathimini ya ya maendeleo ya ujamaa na
utaratibu wa utawala.
Aliongeza kuwa siasa ya ujamaa
na kujitegemea ndio iliyoifanya China kuwa ya pili duniani kiuchumi na
hivi sasa ni ya kwanza kwa mujibu wa tathimini ya Juni mwaka 2014.
Katika mkutano huo kulikuwepo kwa semina ambayo ilihusisha wasomi kutoka vyuo vikuu na baadhi ya viongozi wa chama hicho.
No comments:
Post a Comment