Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo(kushoto) akiongoza kikao cha kujadili Wafungwa waliopendekezwa kuachiliwa kwa Parole(kulia) ni Kaimu Katibu wa Bodi ya Taifa ya Parole, Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa (kulia). Kikao hicho cha siku mbili kimeanza leo Juni 26, 2014 katika Ukumbi wa Mwanza Hoteli, Jijini Mwanza. Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo(hayupo pichani) wakati akitoa hoja ya kufungua Kikao cha kupitia mapendekezo ya Wafungwa waliopendekezwa kuachiliwa kwa Parole( wa kwanza kulia) ni Bw. Francis Stolla akiwa na Wajumbe wenzake wakipitia makabrasha ya mapendekezo hayo. Wajumbe wa Sekretarieti ya Taifa ya Parole wakifuatilia majadiliano katika Kikao cha Bodi ya Taifa ya Parole(wa kwanza kulia) ni Afisa Mwandamizi Kitengo cha Parole, Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Rose Odemba wakifuatilia kwa makini majadiliano ya Wafungwa watakaoachiliwa kwa Parole(katikati) ni Mjumbe wa Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Bruno Pancras(wa kwanza kushoto) ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Merikior Komba. Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole wakiwasili katika Ukumbi wa Mwanza Hoteli tayari kwa Kikao cha Bodi ya Taifa ya Parole kitakachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Juni 26, 2014 katika Ukumbi wa Mwanza Hoteli, Jijini Mwanza(wa kwanza mbele) ni Mjumbe wa Bodi, Bw. Ayub Mwenda toka Ofisi ya Mwendesha Mashitaka Nchini(kushoto) ni Bw. Jonas Tarimo, Mjumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole toka Ofisi ya Kamishna wa Ustawi wa Jamii. Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Mnuo(kushoto) akifanya mahojiano Maalum na Waandishi wa Habari kabla ya kuanza rasmi kwa Kikao cha Ishirini na Sita (26) cha Bodi ya Taifa ya Parole mapema leo Juni 26, 2014. Kikao hicho kitafanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Mwanza Hoteli, Jijini Mwanza(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
………………………………………………………………….
Na; Inspketa Lucas Mboje, Mwanza
Kikao cha Ishirini na Sita
(26) cha Bodi ya Taifa ya Parole kitakachofanyika kwa siku mbili chini
ya Uenyekiti wa Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo kimeanza leo Juni 26,
2014 katika Ukumbi wa Mwanza Hoteli iliyopo Jijini Mwanza ambapo kikao
hicho kitajadili Wafungwa waliopendekezwa na waliopendekezwa kuachiliwa
kwa Parole.Kufanyika kwa kikao hiki ni utekelezaji wa Sheria ya Parole ya Mwaka 1990 ambayo inalenga kupambana na uhalifu nchini na hivyo kudumisha Usalama wa jamii kwa ujumla.
Dhana hii ya Parole ambayo huishirikisha jamii katika kufanikisha Urekebishaji wa wale wanaopata msamaha wa Parole tayari imekwishatumika duniani kwa zaidi ya miaka 300 na imethibitika kwamba ni mfumo sahihi katika kuimarisha Urekebishaji wa Wahalifu na hivyo kuimarisha Usalama wa Jamii.
Hivyo jamii yote kwa ujumla inapaswa kuielewa na kuikubali dhana hii ya Parole na kuachana na tabia ya mtindo wa kumpeleka kila mkosaji gerezani kwani tabia hii husababisha Magereza mengi kufurika na kuwa na msongamano usioruhusu utekelezaji wa programu za Urekebishaji, achilia mbali matatizo mengineyo mengi yatokanayo na hali ya Msongamano.
Hiki ni kikao cha Tano kufanyika chini ya Uenyekiti wa Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo tangu ateuliwe rasmi na Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Taifa ya Parole kuanzia Aprili 24, 2013.
No comments:
Post a Comment