Askofu Mkuu wa KKKT Dk. Alex Malasusa.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Konrad-Adenauer-Stiftung. Baadhi
ya washiriki wa kongamano hilo, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo Dk. Wilbroad Slaa na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Sheria na
Haki za Binadamu Dk. Helen Kijo-Bisimba. na Wilfred Mlay. Meza Kuu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki. Makamu wa Rais Dk. Mohamed Bilal akiagana na mwenyeji wake Askofu Mkuu wa KKKT Dk. Alex Malasusa.
Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO
Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO
………………………………………………………………..
Hussein Makame-MAELEZO
MCHANGO
wa viongozi wa dini katika jamii yoyote ile umekuwa ukipewa nafasi
kubwa hasa katika muktadha wa ujenzi wa jamii bora yenye amani,
maelewano usawa na maendeleo.
Katka
miaka ya hivi karibuni baadhi ya nchi za Ukanda wa Jangwa la Sahara
kama si za Afrika kwa ujumla zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya
migogoro inayochangiwa na ama siasa za nchi husika na tofauti za kidini.
Baadhi
ya migogoro hiyo ni ile inayotokea katika nchi kama za Nigeria, Sudan
Kusini, Somalia ambapo baadhi ya makundi mbalimbali yamekuwa yakipigana
ama kutokana na sababu za kisiasa au kidini.
Kutokana
na hali hiyo viongozi wa dini kutoka nchi za Afrika ikiwemo ukanda wa
Jangwa la Sahara walikutana hivi karibuni kwenye Mkutano wa Kimataifa la
Viongozi wa Kidini kuhamasisha Amani, Demokrasia na Maendeleo.
Katika
mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam, mgeni rasmi alikuwa Makamu wa
Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal huku wadau mbalimbali wa masuala ya
Amani, Demokrasia na Maendeleo walialikwa na kuwasilisha mada
mbalimbali.
Baadhi
ya wadau hao ni viongozi kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Tanzania Labour Party (TLP), Chama cha Wananchi (CUF) na
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Wakati
akifungua mkutano huo Makamu wa Rais Dk. Bilal anawataka viongozi wa
dini kuacha woga na kuwakemea viongozi wa kisiasa wanapokosea kwa
kufanya hivyo wataendeleza amani iliyopo nchini na katika baraza zima la
Afrika.
Dk.
Bilali alisema Serikali ipo tayari kupokea mapendekezo watakayoyatoa kwa
lengo la kudumisha amani na demokrasia kwa maendeleo ya taifa kwa
ujumla na kubainisha kuwa amani inajengwa kwa ushirikiano wa viongozi wa
dini, wanasiasa na wadau wengine katika jamii.
Makamu
wa Rais anasema kutokana na utayari huo ni vyema viongozi wa dini
wakawakumbusha wanasiasa pale wanapokesea ili wajirekebisha na hivyo
kuiepusha jamii kuingia katika uvunjifu wa amani.
Akizungumzia
kongamano hilo Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Dkt. Alex Malasusa anasema lengo la mkutano huo ni kuwakumbusha
viongozi wa dini na wa siasa kuhusu suala la kudumisha amani kwani bila
ya amani hakuna maendeleo.
“Nia
ya mkutano huu ni kuwakumbusha viongozi wa dini kuhusu suala la
kudumisha amani na nafasi ya viongozi wa dini kuombea amani na
kuwakumbusha viongozi wa siasa wajibu wao katika kudumisha amani kwa
sababu bila ya amani hatuwezi kupata maendeleo” anasema Dkt. Malasusa.
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilborad Slaa alikuwa miongoni mwa washiriki waalikwa wa mkutano huo, anasema katika dhana ya maendeleo na amani anakubaliana na hoja kwamba iwapo amani haitakuwepo maendeleo hayawezi kupatikan
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilborad Slaa alikuwa miongoni mwa washiriki waalikwa wa mkutano huo, anasema katika dhana ya maendeleo na amani anakubaliana na hoja kwamba iwapo amani haitakuwepo maendeleo hayawezi kupatikan
“Ni
kweli kwamba iwapo amani haitakuwepo maendeleo pia hayatakuwepo, mimi
nashukuru tumeunganisha amani, demokrasia na maendeleo kwa sababu kila
kimoja kati ya mambo hayo kinategemea kuwepo kwa kingine” anasema Dkt.
Slaa.
Kwa
kutambua umuhimu wa mkutano huo, washiriki kutoka mataifa ya Ethiopia,
Kenya, Nigeria, Afrika Kusini na mweneyji Tanzania hatimaye walitoka na
tamko juu ya mambo yanayoweza kuchangia kuwepo kwa Amani, Demokrasia na
Maendeleo
Mambo
hayo ni katiba za nchi na uhuru wa dini katika ukanda wa Jangwa la
Sahara, Hali tete ya sasa ya uhusiano kati ya wakristo na
waislamu,mchango wa viongozi wa dini katika demokrasia na utawala bora
na tamko la kuangalia fursa za kupunguza umasikini kama njia ya kupata
amani na maendeleo.
“Tunakiri
kwamba tofauti za kidini zimekuwa zikitumiwa vibaya na kwamba matumizi
haya mabaya yamechangia kuvunja amani na hata kupoteza maisha ya watu na
hivyo kuongeza umasikini” inafafanua sehemu ya tamko hilo.
Washiriki
wa mkutano huo pia wamekubaliana kwamba wametambua na kukubali ukweli
kwamba wao kama viongozi wa dini na siasa, ni jukumu lao kujenga na
kuhamasisha thamani ya demokrasia.
Kama
ishara ya matokeo yenye matumaini mema ya mkutano huo na “Tunakiri umoja
kati yetu katika kudumisha amani, kuhamasisha demokrasia na kuhakikisha
tunakuwa na uhakika wa maendeleo endelevu ambayo ni rafiki wa mazingira
katika nchi za Ukanda wa Jangwa la Sahara na Afrika kwa ujumla.
“Tumejitolea
kuhamasisha watu kuwa mstari wa mbele kujenga amani, demokrasia na
maendeleo na kuhamasisha usawa wa kijinsia katika jamii.Kuwahamasisha
wanajamii kujenga daraja katika kufahamiana miongoni mwa watu wa dini na
kujihusisha katika mahusiano ya kidini.
“Kushirikiana
na viongozi wa kisiasa kufanya kazi kwa ajili ya haki ya kijamii na
kiuchumi kama mahitaji ya kujenga amani na kukabiliana na hali tete ya
kidini kabla ya kugeuka vurugu na kupinga majaribio yote yanayofanywa na
mtu au kikundi chochote kutumia vibaya dini na au siasa kwa manufaa
binafsi au ya kisiasa” inasema sehemu ya tamko ambalo lilisainiwa na
washiriki 31.
Washiriki
wa mkutano huo pia wamekubaliana kutambua na au kulaani vurugu zote
dhidi ya jamii yoyote na wameahidi kutumia jukwa lao kama viongozi wa
dini katika kuhamasisha utawala bora.
Mambo
mengine waliyokubaliana ni kuboresha na kuendeleza majukwaa ya
mahusiano au maingiliano ya kidini kwa ngazi zote kwa kuhamasisha ujenzi
wa amani, demokrasia na maendeleo ili kuchangia kupunguza umasikini.
Tamko
hilo limetaka kuhamasisha uelewa wa mahusiano ya kidini katika mfumo
rasmi wa mafunzo kwa viongozi wa dini na kuhamasisha mahusiano endelevu
ya kidini na kukuz dhana ya ukarimu.
Kwa
mujibu wa tamko hilo, washiriki wametaka itambulike ukweli ni kwamba
ujenzi wa amani ni suala mtambuka na ili kuhamasisha uwepo wa amani,
tunatoa wito kwa wadau wote ikiwemo Serikali, taasisi binafsi,
wanasiasa, wasomi na jamii kwa ujumla kuheshimiana na kujenga dhamira ya
kujiletea maendeleo endelevu.
“Kuheshimu
kuwepo kwa tofauti za kidini kama zawadi na isiwe kikwazo cha kupata
amani na kudumisha na kuheshimu kanuni za demokrasia kama mchakato wa
kudumisha haki ya kila mtu” inafafanua sehemu ya tamko hilo.
Kwa
pamoja viongozi hao wamekubaliana kwamba viongozi wa dini wana wajibu wa
kuepuka kuendeleza uungaji mkono katika agenda za kisiasa na kufanyia
kazi mifarakano na machafuko ya kidini.
Mkutano
huo ulidhaminiwa na Shirikisho la Kilutheri Duniani (LWF), Mfuko wa
Konrad Adenauer (KAS), Kanisa la Evangelical Lutheran la Tanzania na
Mission EineWelt, kwa ushirikiano na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania
(BAKWATA).
Taasisi
nyingine katika mkutano huo uliokuwa na kaulimbiu isemayo “Ujenzi wa
Amani, Demokrasia na Maendeleo:Ni Wito kwa Wananchi wa Ukanda wa Jangwa
la Sahara”. Ulihudhuriwa pia na Ofisi ya Mufti ya Zanzibar na Chama cha
Maendeleo ya Asia Tanzania (TADA)
No comments:
Post a Comment