Mkurugenzi
wa Farida Foundation akikabidhi moja ya msaada kwa kaimu Mganga mkuu wa
Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle,Huku wafanyakazi wengine wa
Hospitali hiyo wakishuhudia.
Bi
Farida Abdul Akikabidhi bandeji kwa ajili ya kufungia wagonjwa kwa
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle akipoke Ndoo zitakazotumika kwa ajili ya kuhifadhia uchafu katika Hospitali hiyo,ambazo zilitolewa kama Msaada na Farida Foundation |
Bi
Farida Abdul akimuonyesha kaimu Mganga mkuu wa Hospitali ya Palestina
Dk Hugoline Mselle Vifaa ambavyo vimeletwa kama msaada kwenye Hospitali
hiyo.Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Viti vya magurudumu vitatu ambavyo
vitasaidia kubebea wagonjwa,Bandeji za kufungia vidonda,Ndoo za kuwekea
taka,na vinginevyo.
Hivi
ni viti Vitatu vya kubebea wagonjwa ambavyo vilitolewa kama msaada
kwenye Hospitali ya Palestina(sinza) na Farida Foundation.
Kaimu
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Akimshukuru Bi Farida Abdul kwa
kutoa msaada katika hospitali hiyo na akampongeza kwa moyo wake na
kumsisitiza aendelee Kusaidia kila mara anapopata nafasi ili huduma zao
ziwe bora zaidi kila siku.
Mkurugenzi
wa Farida Foundation Bi Farida Abdul akiongea na vyombo vya habari na
kuelezea ni kwanini ameamua kutoa misaada hiyo katika hospitali ya
Palestina,Amesema kwamba Serikali peke yake haiwezi kufika kwa kila
mgonjwa na hospitali kwa wakati,kwa hiyo inatakiwa kujitoa kwa mashirika
kusaidiana na Serikali ili Hospitalietu Ziweze kuwa na Huduma bora.
Kaimu
mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle ameishukuru
Taasisi ya Farida Foundation kwa misaada waliyotoa kwani itawasaidia
sana kuboresha Huduma zao.
No comments:
Post a Comment