Pages

KAPIPI TV

Wednesday, May 14, 2014

WAKULIMA KATA YA UFULUMA UYUI: TUSILAZIMISHWE KUVIUZIA VYAMA VYA USHIRIKA TUMBAKU YETU


1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa kata ya Ufumula katika mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake inayoendelea  katika mkoa wa Tabora akikagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi ili kuzipatia ufumbuzi, Katibu Mkuu Kinana ameongozana na Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye, Katibu Mkuu huyo kesho ataendelea na ziara hiyo katika wilaya ya Sikonge, Wakulima wa kata ya Ufuluma wamelalamikia kulazimishwa na viongozi wa vyama vya ushirika kuwalazimisha kuuza tumbaku yao katika vyama hivyo hata kama sio wanachama wameomba wasisumbuliwe ili waweze kuuza tumbaku yao mahali popote bila kubughudhiwa. Jambo ambalo limeungwa mkono na mkuu wa mkoa wa Tabora Mh. Fatma Mwassa(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-UYUI-TABORA) 3 Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika kata ya Ufuluma wakati wa mkutano wa hadhara kijiji hapo leo.  5 6Mwenyekiti wa halmashauri ya Uyui Bw. Said Ntahondi akizungumza na wananchi wa kata ya Ufuluma wakati wa mkutano wa hadhara. 7Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh. Fatma Mwassa akizungumza na wananchi wa Kata ya Ufuluma kuhusu tatizo la kubiwa kwa fedha zao zinazotokana na uuzaji wa tumbaku. 9Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na mmoja wa vijana ambaye  alionekana akitoka kuchota maji na mkokoteni wa kukokota na Ng'ombe 10Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiingia katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Mwanakiyungi Isike ili kukutana na waalimu. 11Waalimu wa shule mbalimbali wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ili kumsikiliza. 12Waalimu mbalimbali wakiwa katika mkutano huo. 13Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na waalimu wa shule mbalimbali katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa wa Mwanakiyungi Isike. 14Mwalimu Petro Sizya akuliza swali katika mkutano huo.
3aKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakikagua maabara katika shule ya sekondari ya wasichana ya Ndono wilayani Uyui aliyeongozanana naye ni Mhandisi wa ujenzi wa wilaya ya Uyui Bw. Stephen Nyanda.

No comments: