Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mei 16, 2014 katika viwanja vya Mwananchi Squire mjini Urambo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi huku akijadiliana nao njia ya kuzitatua katika mkoa wa Tabora
Maelfu ya wananchi wakimsikiliza Kinana kwenye mkutano huo
Kinana akiinuliwa baada ya kusimikwa uchifu wa Wanyamwezi kabla ya kuhutubia mkutano huoKatibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisiitiza jambo akihutubia maelfu ya Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mei 16, 2014 katika viwanja vya Mwananchi Squire mjini Urambo, akiwa na Kinana katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi huku akijadiliana nao njia ya kuzitatua katika mkoa wa Tabora Kinana akimvisha kofia ya usalama, Katibu wa CCM kata ya Ukondamoyo, Barakabraka wakati akimkabidhi pikipiki . Jumla ya pikipiki 16 zimetolewa na Sitta na Mama Sitta



Mnara uliopo kwenye shamba la kituo cha kilimo cha Umwagiliaji wa matone
Kinana akiangalia mhindi kwenye shamba darasa la kilimo cha mwagiliaji kwa matone la Kapilula, Urambo
Kinana akitazama mahindi yanavyopata maji kupitia matone, katika shamba darasa la Kapilula, Urambo
Mbunge wa Viti Maalum Mama Margareth Sitta akitazama mahindi yalivyozaa kwenye shamba hilo
Kinana katika wodi ya wazazi ya Yuwilindila
Muuguzi Mkunga wa Zahanati ya Izenga, Urambo mkoani Tabora, akimuonyesha Kinana hifadhi ya dawa
No comments:
Post a Comment