Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUMA Energy Tanzania, Bw. Phillipe Corsaletti akiongea katika uzinduzi wa Vilainishi vya Castrol vilivyoendana na uzinduzi wa kituo kipya cha Mafuta kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Wageni na wafanyakazi wa kampuni
ya PUMA Energy Tanzania wakifuatilia uzinduzi wa Vilainishi vya Castrol
vilivyoendana na uzinduzi wa kituo kipya cha Mafuta kilichopo Masaki
jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa Kituo Kipya cha Mafuta kilichopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Gari litakalotumiwa katika mashindano ya Magari yanayotarajia kufanyika Mwishoni mwa wiki.
Wateja wakipatiwa huduma na wafanyakazi wa kampuni ya PUMA Energy Tanzania.
Meneja
Mauzo wa Vilainishi vya Castrol, Gilbert Chacha akizungumza wakati wa
uzinduzi ambapo alisema kuwa Vilaainishi vya Castrol vina ubora wa
kimataifa na hutumika katika magari, viwanda, meli, ndege. Kwa sasa wana
aina mbili za Vilainishi hivyo Castrol GTX 20W50 na GTX Diesel 15W40.
Pembeni yake niMshereheshaji Shebe Machumani na dereva wa gari la
Mashindano.
Meneja wa Usalama wakati wa Kazi wa Kampuni ya PUMA Energy Tanzania, Jonathan Mmari akizungumza machache.
Walioko
mbele kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya PUMA Energy
Tanzania, Dkt. Ben Moshi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUMA
Energy Tanzania, Bw. Phillipe Corsaletti wakiwa na wageni waalikwa
wakati wa uzinduzi wa Vilainishi vya Castrol vilivyoendana na uzinduzi
wa kituo kipya cha Mafuta kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni
ya PUMA Energy Tanzania, Bw. Phillipe Corsaletti akionyesha picha ya
sanamu itakayotumika kutambulisha vilainishi vya Castrol wakati wa
uzinduzi wa Vilainishi vya Castrol vilivyoendana na uzinduzi wa kituo
kipya cha Mafuta kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam. Pembeni yake
ni Mshereheshaji Shebe Machumani.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni
ya PUMA Energy Tanzania, Bw. Phillipe Corsaletti na Mshereheshaji Shebe
Machumani wakionyesha vilainishi vya Castrol.
Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
No comments:
Post a Comment