"VIONGOZI ACHENI MARUMBANO MJADILI NA KUTAFUTA MAENDELEO YA JAMII"-KINANA
Mh.
Samwel Sitta Mbunge wa jimbo la Urambo Mashariki na Waziri wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisalimiana na Profesa Juma Kapuya
Mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi leo asubuhi katika kijiji cha Usindi
kata ya Ushokora wilayani Kaliua wakati wa pamokezi ya Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitokea Wilaya ya Urambo.Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Prisca
Kaholwe Ofisa mtendaji wa kijiji cha Uhuru wilayani Urambo wakati
alipokagua ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho.Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na viongozi mbalimbali
wa a CCM wilayani Kaliua wakielekea kwenye ukaguazi wa ujenzi wa nyumba
za watumishi wa Zahanati ya Kijiji cha Usindi Kata ya Ushokora
wilayani Kaliua.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa nyumba za watumishi wa zahanati ya kijiji cha Usindi.
No comments:
Post a Comment