Pages

KAPIPI TV

Friday, April 25, 2014

MILIONI 10 KUSAIDIA KUNUNUA VITANDA NA MAGODORO HOSPITALI YA RUFAA MAWENI KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma
Kiasi cha shilingi Milioni 10 zinatarajia kutumika kununua vitanda na magododoro katika Hospitali ya Rufaa  Maweni, ikiwa ni sehemu ya kupunguza changamoto hiyo kwa  wagonjwa .
 
Akifafanua hilo Meneja Kanda Magharibi  Benki ya   NMB Abraham Agustino alisema lengo la serikali ni kuboresha huduma za jamii. Hivyo  kwa kushirikiana na asasi za kiraia  wanachangia fedha hizo ,ikiwa ni sehemu ya sera ya uchangiaji,ambapo wanatoa aslimia moja ya faida  kila mwaka kuboresha huduma za jamii.
 
 
Alisema wadau wa maendeleo hawana budi kuunga mkono sera ya uchangiaji wa huduma za kijamii,ikiwa ni njia ya kuonyesha uzalendo wa taifa lao,huku akihamasisha wananchi watumie huduma ya chapchap ambayo ni tija kwa wakazi waishio vijijini.
 
 
Kwa Upande wa mgeni rasmi Ramadhan Maneno  ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya kigoma kwa niaba ya mkuu wa mkoani hapa Lt.Issa Machibya, aliipongeza tasisi hiyo kwa kitendo chake cha kujali wagonjwa  ambapo kimaendeleo kigoma inahitaji fursa maalum ili iendane na ulimwengu wa leo.
 
 
“leo tunashuhudia uzinduzi rasmi ya benki hii tangu ianze kufanya kazi  mwka 2000 hadi leo , wananchi tumieni fursa hii, muondokane na umaskini,tumieni  vikundi mpate mikopo kulingana na tija yenu,msikae majumbani kujifungia tembeeni mbaini fursa” alidai Ramamdhan Maneno .
 
Naye Mganga Mkuu wa mkoani hapa Leonard Subi alisema ,hospitali hiyo inachangamoto mbalimbali za huitaji hasa  vifaa tiba na wataalamu wa vitengo vya idara ikiwemo upande wa mifupa,sikio na wasomaji wa Ex-Rey,ambapo kwa sasa vitengo hivyo vinasuasua.
 
 
Baadhi ya wananchi  kwa nyakati tofauti walihojiwa na gazeti hili  juu ya msaada huo Mariam Issa na Kasim Msenegal walisema faida itakuwepo ikiwa utawala wa hospitali hiyo itazingatia usimamizi bora wa matumizi sahihi na si vinginevyo,huku wataka kipaumbele iwe  wodi ya wazazi na watoto.ambapo kwa sasa baadhi ya wagonjwa walala wawil iwawili na wengine chini.
 
Walisema  uongozi ujipime kutumia fursa hizo kwa walengwa kutokana na hulka ya kushindwa kutumia baadhi ya misaada huku wakitolea  mfano msaada wa magodoro na neti zilizowahi tolewa na asasi ya Kicora ya kigoma hazitumiki na hatimaye mgonjwa akilazwa huenda na neti yake.

No comments: