Na Magreth Magosso,Kigoma
IMEELZWA kuwa,asilimia 6 ya watoto walio chini ya umri wa
miaka mitano Mkoa wa Kigoma wapo hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kutokana
na kukosa chanjo ya kuzuia magonjwa mbalimbali ukiwemo uti wa mgongo na kuhara.
Akifafanua hilo Mganga Mkuu wa Mkoa Leonard Subi kwenye uzinduzi wa wiki ya chanjo kitaifa
ambapo hapa imezinduliwa katika wilaya ya Uvinza kata ya
Kazulamimba,ikiwataka jamii,familia na watendaji wa vijiji kila mtu kwa nafasi
yake ahamasishe ili kutimiza lengo la taifa 95% ya watoto husika wawe wamepatiwa chanjo hiyo.
Alisema lengo la kutoa chanjo hiyo ni kuondoa ugonjwa wa
kupooza,kifua kikuuu,kifadulo,kichomi,kuhara kwa maslai ya kupata viongozi bora
siku za usoni kutokana na watoto waliopata chanjo zote na kwa wakati
wanauhakika wa kuishi maisha marefu na yenye siha njema sanjari na kujengeka
vyema kiakili.
“Mwaka 2012 ,91% ya watoto walio chini ya umri wa miaka
mitano walipatiwa chanjo na 2013-94% ,walichanja,shida ipo kwenye 6% wana
hatari ya kupata maradhi ya mlipuko ,mkoa wetu
unapakana na nchi ambazo zenye utata wa magonjwa ya mlipuko” alibainisha
Dkt.Subi.
Akisemea hilo Mgeni rasmi
pia mkuu wa wilaya ya kigoma Ramadhan Maneneo kwa niaba ya Mkuu wa
mkoani hapa,Lt Issa Machibya aliwaasa
viongozi wa dini zote mbili waislamu na wakristo sambamba na viongozi wa
siasa wawajibike kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa chanjo hizo kwa ngazi
ya kitongoji na kaya.
Maneno alisema jamii itumie fursa hiyo na iachane na fikra
potofu ya kudhani chanzo inaondoa uzazi wa muhusika,bali ni chachu ya kuboresha
na kujenga akili imara ya mlengwa na kupunguza idadi ya vifo , vifo vya
watoto waliochini ya umri wa miaka
mitano vimepungua kutoka vifo 51 katika vizazi hai 1,000 Hadi kufikia vifo 11
kwenye vizazi hai 1,000.
Naye Mkuu wa wilaya ya uvinza Hadija Nyembo aliwataka wakina
baba waachane na mfumo dume ili washiriki zoezi la kupeleka watoto wao
kliniki wakapatiwe chanjo kutokana na
kina mama kuwa na majukumu mengi ya kifamilia,hivyo hawana budi kushiriki zoezi
hilo litakaloishia 30,4,2014.
No comments:
Post a Comment