Na Magreth Magosso,Kigoma
Wakazi waishio vijiji vilivyopo katika majimbo ya Kigoma Kaskazini na Kusini wameomba uongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kuangalia upya viwango vilivyowekwa kwa ajili ya upigaji picha kwa wanafunzi wa darasa la saba viweze kwendana na hali halisi ya maisha ya wakazi hao.
Baadhi ya wakazi wakiwemo Rahma Hamza na Mariamu Issa hao wamesema kuwa hali halisi ya maisha kwa sasa ni magumu kutokana na hali ya vipato kutokidhi mahitaji ya nyumbani hivyo viwango vilivyowekwa havikuzingatia hali ya maisha ya wakazi wa eneo husika.
Walisema kuwa awali kiwango kilichokuwepo kwa kila mwanafunzi kilikuwa ni shilingi 2500 ambapo kiwango hicho kimepanda na kufikia 5000 kwa kila mwanafunzi ni lazima maamuzi yanayofanywa na viongozi yazingatie hali ya kipato kwa kila mwananchi bila kujali wale wenye uwezo.
Aidha Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Vigele tarafa ya Nkungwe kata ya Mahembe bw. Alphonce Mbasa alisema kuwa kutokana na ongezeko hilo la asilimia 100 limesababisha wazazi wengi kushindwa kulipia kiasi hicho ambapo hadi sasa ni wanafunzi watatu ndio waliolipia kati ya wanafunzi 45.
“ wazazi wanalalamikia ongezeko hilo na wana watoto zaidi ya watatu na hali ya kipato kwa siku anatumia chini ya shilingi 1000 anatakiwa kulipia 15,000, hivyo inakuwa ngumu kumudu gharama hizo”alisema Mbasa.
Mbasa alisema kuwa licha ya gharama hizo kupanda lakini pia taarifa hizo hazikuja mapema ili wazazi wajiandae kukabiliana na ongezeko hilo ambapo hatua hiyo ilianza machi 10 na inatarajiwa kumalizika ifikapo machi 15 ambapo wanafunzi wengi hawata pata fursa ya kupiga picha.
Amesema kuwa kutokana na kauli za viongozi walidai kuwa awali picha zilizopigwa hazikuwa katika ubora na viwango vinavyotakiwa na hivyo kuamua kuleta mtu kutoka mikoa ya jirani kwa ajili ya kazi hiyo sambamba na kupanda kwa gharama za utengenezaji wa picha hizo.
Hata hivyo Buchumi Nashoni Mratibu elimu kata, Kata ya Mkigo alisema kuwa taarifa zilizofika ofisini ni kuwepo kwa mtu rasmi kwalengo la kupiga picha kwa wanafunzi wa shule zote za halmashauri ya Wilaya.
Alisema kuwa Changamoto iliyopo ni walimu wakuu wa shule kuingia katika mgongano wa matumizi ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya matumizi ya shule kuingizwa katika mchakato huo wa upigaji picha jambo ambalo litakwamisha baadhi ya shughuli zilizotakiwa kufanya kwa kipindi hicho.
Aidha amesema kuwa halmashauri ilitakiwa kuwashirikisha walimu ili taarifa hiyo ifikishwe katika kamati ya shule na kuwashirikisha wazazi ili wawe na maamuzi ya kiwango wanachoweza kukimudu.
Sanjari na hilo utaratibu uliowekwa haukuzingatia taratibu za ufundishaji wa vipindi kwa walimu ambapo kwa siku hiyo italazimika kusimama kwa baadhi ya vipindi vya masomo.
Akizungumzia hilo Afisa elimu wilaya shule za msingi Maya Mlangi alisema awali picha zilizopigwa na walimu wa shule hazikuzingatia viwango na hivyo kusababisha Halmashauri kuingia katika hasara ya kurudia mchakato huo na hivyo kuona ni vyema awamu hii kuleta mtaalamu wa kupiga picha kutoka Jiji la Mwanza.

No comments:
Post a Comment