Pages

KAPIPI TV

Thursday, March 13, 2014

TUWASA WAENDELEA KUKAMATA WIZI WA MAJI

Operesheni maalumu ya kusaka wezi wa maji ya Mamlaka ya Maji Safi  Tabora mjini TUWASA ambapo katika zoezi hilo maafisa wa Serikali na wale wastaafu ndio waliokamatwa wakihujumu na kuiba huduma hiyo ya maji kwa kujiunganishia isivyo halali.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji Safi Tabora mjini  Tuwasa  Bw.Mkama  Bwire akizungumza na mmoja wa wateja wa Mamlaka hiyo ambaye alikamatwa akihujumu huduma ya maji kwa kujiunganishia kinyemela
Baadhi ya waliokamatwa wakiiba maji walikuwa wakitumia njia za aina mbalimbali kujitetea hatua ambayo ilikuwa ikiwachosha maafisa wa Tuwasa ambao waliambatana na Mkurugenzi wao katika msako huo mkali.

Zipo baadhi ya nyumba ililazimika hata kutumia mbinu za ziada katika kufichua uharifu ambapo Meneja Masoko wa Mamlaka ya Tuwasa Bw.Benard Biswalo alionekana akiruka uzio ilimradi aingie ndani ya nyumba hiyo ambayo wenyewe walikataa kufungua milango kutokana na uhalifu waliokuwa wakiufanya.



No comments: