Pages

KAPIPI TV

Thursday, March 13, 2014

KIGOMA WATAKIWA KUWA MAKINI NA WANASIASA WANAOANZISHA VYAMA WAKATI WA KUELEKEA KWENYE UCHAGUZI

Na Magreth Magosso,Kigoma

WANANCHI wa Mkoa wa Kigoma wameaswa waache hulka ya kushabikia  vyama vya siasa vinavyozuka hivi sasa,kutokana na waasisi wake ni miongoni mwa walioharibu kwenye vyama vyao vya awali.

Akithibitisha  kauli hiyo Katibu wa N.R.A Taifa Fadhili Kiswaga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kigoma ujiji, alisema wananchi watajuta kupokea vyama  holela pasipo kufanya uchunguzi na kubaini  kiini cha chama husika.
 

“Shida jamii haiumizi kichwa, viongozi wanaoanzisha vyama nyakati za uchaguzi ni mamluki wanaobomoa  vyama  vinavyokemea maovu ya serikali ili wahudumiwe wao, watajuta na tabia ya kufuata utashi  wa mtu anayevaa ngozi ya kondoo eh! kigezo utendaji “alibainisha Kiswaga.

Alisema chama cha CHADEMA ambacho kimeshika madaraka ya Udiwani kata ya Mwandiga tangu 1994 hadi leo ,lakini wananchi wana adha ya maji safi na salama  miaka dahari sanjari na  soko chafu, ambapo wafanyabiashara wamejenga vibanda kwa kutumia mifuko ya Plastiki maarufu  Rambo.

Hata hivyo kata ya Mwandiga ni miongoni mwa kata ya Jimbo la Mh,Zitto Kabwe ambaye ametawala kwa miongo kadhaa pasipo kuondoa changamoto ya maji na soko .huku akisisitiza chama cha Alliance For Change Transiparecy ( A.C.T) ni sehemu ya viongozi 17 wasiofadhirika kihistoria kwenye vyama vyao vya awali.

Jacob Ruvilo na Buchumi Nashoni ambao ni wadau wa Siasa  walisema Wanasiasa wanapaswa kukuza demokrasia kwa hoja na kuvumiliana mapungufu baina yao ili kuondoa utashi binafsi unaoangamiza vyama vya upinzani kutokana na  uchu wa madaraka unaopelekea,ukanda na udini ambao ni janga kwa watanzania.

Walisema ukanda  na udini sio tatizo  kinachogombaniwa ni nyadhifa, kama dhima ni kuwatumikia wananchi ni lazima kuongeza nguvu kwenye vyama dhaifu ambavyo vina sera makini na si kuanzisha chama ambapo ni  gharika kwa vyama vya upinzani.

Naye Katibu wa kanda ya kati chama cha chadema Alphonce Mbasa    alisema, kuanzishwa kwa chama hicho sio sababu ya chama cha CHADEMA kufa na kupoteza hadhi ya kuendelea kutawala katika maeneo ya mkoa wa Kigoma
 

Lengo la ilani za vya siasa ni kutaka kuwakomboa wananchi katika kuwatatulia matatizo mbalimbali yakiwemo kuboresha miundombinu ya maji pamoja na barabara na sio kuanzisha vyama mbadala ambavyo vinaonekana kuwa na  mlengo wa mtu Fulani licha ya mapungufu aliyonayo.

No comments: