.Na Magreth Magosso,Kigoma
SHUGHULI za uvuvi zinazofanywa katika
Ziwa Tanganyika zipo hatarini kutoweka ,kutokana na sintofahamu ya
kuongezeka kwa matukio ya ujambazi katika ziwa hilo.
Hali hiyo
inatokana na kupungua kwa Vipe na zana za uvuvi unaosababishwa na wizi
unaofanywa na majambazi wanaotoka DRC-Congo ambapo hadi sasa mvuvi
mmoja ametekwa na vipe 18 sanjari na zana zake bado havijapatikana.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wavuvi Mkoani hapa Ramadhan Kanyongo alisema,changamoto
hiyo ni vita ya kitaifa kutokana na serikali kutoliwekea kikosi kazi cha
kudumu ili kiweze kushiriki na maeneo ya ukanda wa ziwa hasa eneo la
Lubengela,kagunga,kalya,nyamhoza na mgambo,ili kudhibiti maficho na njia
mtambukwa kwa majambazi.
“ askari wa ziwani hawana mafuta ya
kutosha kwenye boti za kufanya dolia katika mipaka na maeneo nyeti
yanayotumiwa na wahalifu,wanakuwa ombaomba, serikali wakilifumbia macho
nchi itakuwa na wahalifu vijana wanaokosa ajira kutokana na vipe kuibwa
kila wakati machi ,3,2014 vipe 10 ajira 60 zimeisha” alibainisha
Kanyongo.
Katibu wa Umoja huo Francis John alisema serikali
ifanye mazungumzo na serikali ya Congo DRC waweke mkataba wa kudhibiti
hatma ya mipaka inayotumiwa na wahalifu katika njia ya maji ili kuepuka
suala la uvamizi wan chi baina yao pindi wanapofukuzana na majambazi
ziwani.
Paulo Samweli Mvuvi wa Kibirizi alisema neno la ujirani
ni chachu ya watu wa Congo na baadhi ya wadau wa uvuvi wa hapa
kushiriki matukio ya uhalifu ambapo zana za wavuvi zinapatikana
DRC-Congo na wakifuata hutozwa kwa dola 500 kwa kila zana ya uvuvi .
“uaminifu
ni silaha ya kufanikisha janga hili,serikali iweke nguvu kwa askari
polisi na jeshi la wananchi(JWTZ) kigoma kutokana na jiografia yake
,ililea wakimbizi tangu 1962 hivyo, wanajua mazingira na udhaifu wa
majeshi yetu” alidai Mratibu wa Wavuvi Maiko Kiwele.
Kutokana na
kukithiri kwa tatizo hilo Mkuu wa mkoa Kigoma Luten Kanal Mstaafu Issa
Machibya alisema ni lazima zana za wavuvi zilizoko wilaya ya Kalemee
zitarudi kwa wamiliki ikiwa ni pamoja na kukomesha vitendo hivyo katika
ziwa hilo,familia 60 zinathirika kwa sasa na njaa kutokana na faida
zao.
Alisema kuwa kwa kushirikiana na wananchi, wavuvi na vyombo
vya usalama tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kuendesha
msako wa kuwakamata wahamiaji wanaoishi kinyume cha sheria na
kuwarudisha katika nchi zao.
Awali wilaya ya kalemee mkoa wa
Lubumbashi ni sehemu kongwe kwa kuhifadhi zana za wizi unaofanywa na
baadhi ya askari jeshi wa waasi ambao wanatumia mwanya wa ujirani mwema
kwa kushiriki kuangamiza shughuli za uvuvi kigoma hadi leo vijana 60
hawana ajira kutokana na kuibwa kwa vipe 10 na kutoweka na mvuvi.
|
No comments:
Post a Comment