Katibu
wa chama cha waandishi wanawake (Women in Media Organization - WMO)
tawi la mkoa wa Singida, Awila Silla, akitoa taarifa yake ya msaada wa
mizinga 80 kwa vikundi vinne vya wafuga nuki wanawake kutoka wilaya ya
Singida na Ikungi.
Mkuu
wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akizungumza kwenye hafla ya
kukabidhi msaada wa mizinga ya nyuki kwa vikundi vinne vya Wanawake
wafuga Nyuki.Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi na kulia
ni mwenyekiti wa WMO Evarista Lucas.
Mkuu
wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone (wa pili kulia) akikabidhi mzinga
wa Nyuki kwa wawakilishi wa vikundi vinne vya wafuga Nyuki wa wilaya ya
Singida na Ikungi.Wa kwanza kulia ni Afisa Maliasili mkoa wa
Singida,Charles Kidua.
Mkuu
wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, (wa pili kulia walioketi) akiwa
kwenye picha ya pamoja na wanakikundi wa ufugaji nyuki kutoka wilaya ya
Singida na Ikungi.Wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa WMO Evarista
Lucas.Kushoto ni afisa maliasili mkoa Charles Kidua na anayefuata ni
mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
CHAMA
cha Waandishi wa Wanawake (Women in Media Organization – WMO) mkoani
Singida kimetoa msaada wa miziga 80 ya nyuki ya kisasa, kwa vikundi vine
vya wanawake wa halmashauri ya Singida na Ikungi.
Mizinga hiyo ya kisasa iliyotengenezwa na SIDO ndogo mjini hapa, inakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi.
Hayo
yamesemwa hivi karibuni na Katibu wa WMO mkoani Singida, Awila Sill
wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi mizinga hiyo ya kisasa
iliyofanyika kwenye viwanja vya SIDO mjini Singida.
Amesema
vikundi hivyo ni kutoka vijiji vya Masweya na Muhintiri vya wilaya ya
Ikungi na Ilongero na Nduamughanga vya halamashauri ya wilaya ya
Singida.
Awila
ambaye ni mwandishi wa habari wa gazeti la mwananchi na the citizen
mkoani hapa, alisema mizinga hiyo kila moja una uwezo wa kutoa/kuzalisha
lita 20 na bei ya lita moja kwa sasa ni shilingi 10,000.
“Wanakikundi
wote,tumeishawapatia mafunzo ya ufugaji bora wa nyuki.Kwa hiyo
tunayoimani kuwa mbele ya safari,wanakikundi hawa watanufaika na msaada
huu na kwa vyo vyote,watajikomboa kiuchumi”,amesema Awila.
Katika
hatua nyingine, Katibu huyo alitumia fursa hiyo kuishukuru serikali
kupitia wizara ya maliasili na utalii kitengo cha mfuko wa misitu nchini
kwa kukipatia WMO ruzuku ya zaidi ya shilingi 14.4 milioni.
Kwa
upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo, mkuu wa mkoa wa Singia, Dk.
Parseko Vicent Kone, ameziagiza halmashauri za wilaya na manispaa,
kuongeza juhudi katika kuendelea kuibua vikundi vingi zaidi vya ufugaji
nyuki.
Aidha,
ameziagiza kuwaondoa mara moja wavamizi wa misitu na hasa kwenye misitu
ya vijiji vya Mgori, Minyughe, Mlilii, Sekenke/Tulya, Wembere, Chaya na
maeneo mengine yaliyoharibiwa.
“Halmashauri
mnalo jukumu la kuzuia ukataji miti ya asili kwa ajili ya kukaushia
tumbaku, wakulima wa tumbaku wanapaswa kupanda miti kwa ajili ya
matumizi yao”,amesema Dk.Kone.
No comments:
Post a Comment