Afisa
uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde(kulia)akiongea na waandishi wa
habari(hawapo pichani)wakati wa droo ya promosheni ya ‘Mimi ni Bingwa’
iliyochezeshwa Jumanne jioni katika ofisi za makao makuu ya Airtel. Bw.
Rashid Jackob Kagombola, mkazi wa Bukoba mkoani Kagera alitangazwa
mshindi wa shilingi milioni 50. Kushoto ni Mkaguzi mwandamizi kutoka
Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Bw. Bakari Maggid.Afisa
Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde (kulia) akimwonyesha Mkaguzi
mwandamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Bw. Bakari
Maggid namba ya katika droo kubwa ya promosheni ya ‘Mimi ni Bingwa’
iliyochezeshwa Jumanne jioni katika ofisi za makao makuu ya Airtel. Bw.
Rashid Jackob Kagombola, mkazi wa Bukoba mkoani Kagera alitangazwa
mshindi wa shilingi milioni 50.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya mawasiliano ya Airtel Tanzania kupitia promosheni yake ya ‘Mimi ni
Bingwa’ imemfanya Bw. Rashid Jacob Kagombola, mkazi wa Bukoba mkoani
Kagera kuwa tajiri baada ya kujishindia milioni 50 katika droo kubwa ya
bahati nasibu iliyochezeshwa na kampuni hiyo mwishoni mwa wiki jijini
Dar es Salaam.
Akimtangaza
mshindi Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema “Leo
hii tumefikia mwisho wa promosheni yetu ya ‘Mimi ni Bingwa’ ambayo
imewanufaisha watanzania walio wengi.
Limekuwa ni zoezi lenye mafanikio
makubwa likiwa na idadi kubwa ya wateja wakijiunga katika promosheni na
kujishindia zawadi katika vipengere tofauti.
“Ningependa
kuwashukuru wateja wetu kwa kushiriki katika promosheni hii tangu
ilipoanza mwishoni mwa mwezi November mwaka jana. Airtel bado mipango
mingine mingi inakuja, tukilenga kuendelea kurudisha kile tulichonacho
kwa wateja wetu na kuisaidia jamii inayotuzunguka kukuza viwango vyao
vya kuishi,” alisema Mmbando.
Alisisitiza
kuwa mbali na zawadi kubwa ya milioni 50 kutolewa, washindi wa awamu ya
pili na ya tatu wa safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia
mechi ya moja kwa moja ‘live’ ya klabu ya Manchester United wataondoka
nchini mwezi huu pale klabu hiyo ikitarajia kucheza tena katika uwanja
wa Old Trafford.
Kwa
upande wake, milionea mpya akizungumza kupitia simu kutoka Bukoba
aliipongeza Airtel Tanzania kwa kuanzisha promosheni zinazosaidia
kuyabadilisha maisha ya wateja wake na kuleta mabadiliko chanya katika
jamii na nchi nzima kwa ujumla.
“Hii
ni miujiza inayotokea maishani mwangu. Siwezi kuamini nami nimeingia
katika orodha ya mamilionea Tanzania. Ni kama ndoto kwangu imekuwa kweli
sababu ya Airtel. Naishukuru Airtel Tanzania kwa msaada wao si tu kwa
wateja wake bali pia kwa jamii yote inayoizunguka. Hizi milioni 50
hakika zitabadilisha maisha yangu kabisa na zawadi nitakayoipatia Airtel
ni kubaki kuwa mteja wao mwaminifu wakati wote,” alisema Bw. Kagombola.
“Nimejiunga
na promosheni ya Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ tangu ilipoanza mwezi
November, na nilikuwa nikicheza pale tu nitakapokuwa na salio la
kutosha. Ilikuwa ni changamoto kuweza kupata pesa ili kuongeza salio la
muda wa maongezi, lakini siwezi kuamini leo hii mimi ni milionea!
Shukrani ziende kwa promosheni ya Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ kwa
kubadilisha maisha yangu,” aliongeza.
Promosheni
ya Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ imeanza mwezi Novemba mwaka jana, ikiwa ni
matokea ya ushirikiano katika ya klabu ya Manchester United na kampuni
hiyo ya simu, haikulenga kuwazawadia wateja pekee, bali pia
kuwaunganisha washiriki na soka la kimataifa na kusaidia kukuza hari ya
michezo miongoni mwa watanzania.
Wakati
wa promosheni hiyo, washiriki wawili wa Mimi ni Bingwa walizawadiwa
shilingi milioni 2 kila siku, wawili wakijishindia shilingi milioni 5
katika droo za kila wiki na mmoja kujishindia tiketi mbili za safari
iliyogharamiwa kila kitu kwenda Old Trafford.
No comments:
Post a Comment