Pages

KAPIPI TV

Sunday, March 16, 2014

THRD YAWAPA SOMO WAANDISHI WA HABARI WANAOFUATILIA MJADALA WA RASIMU YA KATIBA BUNGENI

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais Muungano ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bi.Samia Hassan Suluhu akiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa habari wanaofuatilia Bunge maalumu la Katiba mjini Dodoma muda mfupi mara baada ya kufungua Semina ya siku moja iliyoitishwa na Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu nchini THRD iliyofanyika Dodoma Hotel.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu Bw.Onesmo Olengulumwa akitoa maelezo kuhusu kutotambulika kwa Watetezi wa haki za binadamu kwenye rasimu ya katiba mpya wakati wa semina hiyo.
Kutoka kulia ni Kuringe Mongi  wa Channelten  na  Mussa Juma wa  gazeti la Mwananchi ni miongoni mwa baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika semina ya kuwajengea uwezo kuhusu vipengele mbalimbali ambavyo havikupewa umuhimu katika rasimu ya Katiba mpya vikiwemo vya Haki za binadamu na watetezi wa haki hizo kwa ujumla.
Kutoka kulia ni Mpiga picha wa gazeti la Mwananchi Bw.Emmanuel Herman
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Bi.Samia Hassan Suluhu akifungua Semina ya siku moja inayohusu nafasi ya Watetezi wa haki za binadamu na asasi za kiraia katika Katiba mpya,iliyofanyika mjini Dodoma ambapo Bi.Samia ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa Bunge maalumu la Katiba aliwataka waandishi wa habari kuandika habari zenye maslahi kwa wananchi na si kushabikia masuala ya Muungano pekee. 







No comments: