Na Magreth
Magosso,Kigoma
IMEFAHAMIKA kuwa,Ukosefu wa Maji kwa wakazi wa
Mwambao wa Ziwa Tanganyika Mkoa wa Kigoma limekuwa sugu ,hali inayosababishia
wanawake wa wanaoishi katika vijiji husika
kuvunjika kwa ndoa zao .
Changamoto hiyo inayowakabili wakazi hao inatokana
na viongozi husika kutokuwajibika ingawa vijiji hivyo vipo pembezoni mwa ziwa Tanganyika
hali inayochangia jamii iwe sehemu ya uchafuzi wa mazingira ya ziwa hilo lenye
rasilimali ya madini ya gesi,samaki ,dagaa wa aina mbalimbali.
Mkazi wa Kalalangabo, Kabwe Mzee alisema
kumekuwa na mgogoro wa mahusiano
hasi kati ya mke na mume kwa kuwekeana dhana potofu kuwa huenda mkewe hakuwa
kisimani kusubiri maji na hivyo kupelekea ndoa zao kuvunjika.
“kuna korongo moja ambalo kijiji kinategemea maji ya
kunywa na kupikia sasa nyakati ya kiangazi hali huwa mbaya zaidi kutokana na foleni kubwa kina mama
huamka alfajiri kuwahi foleni hapo sasa baba haelewi kama si kichapo ni kumtanga talaka
tu” alidai Mzee.
Mwatano Shaban na Sophia Steven Mkazi wa Ilagala alisema wanawake wamekuwa wahanga wa
changamoto hiyo kutokana na wanaume kutojali umbali wa eneo la maji safi na
wingi wa hitaji kwa wakazi husika, wanachojua wao ni kutoa adhabu ya kipigo na
talaka hali inayosababisha watoto waishi maisha hatarishi.
Diwani wa kata ya Kalalangabo, Maganga Patrick
alisema awali kata ilikuwa na bomba eneo la kolongo ni mita 100 kutoka kijijini hapo, lakini liliharibika
kitambo hali inayowalazimu kusubiri foleni kisimani na wanaume wasio na uelewa wa
mambo huwapa talaka wake zao hatimaye watoto wanakosa mapenzi ya wazazi wawili.
Makem Shaban na Maria Joackim wakazi wa kata ya
Kalya kwa nyakati tofauti walisema serikali imeshindwa kuwajibika kwa wazi wa
mawambao wa ziwa Tanganyika na wamekuwa wakiwatumia nyakati za uchaguzi ili
kutimiza ndoto zao na si kutatua kero za wananchi wake hali inayochangia wakazi
wa mwambao wa ziwa hilo kuwa nyuma ki
maendeleo.
No comments:
Post a Comment