Mkurugenzi
wa manispaa ya Singida, Joseph Mchina akitoa taarifa yake ya
utekelezaji mbele ya kikao maalum cha baraza la madiwani. Wa pili kulia
ni Mustahiki meya wa manispaa ya Singida na Sheikh wa mkoa wa
Singida,Salum Mahami.Wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa CCM manispaa ya
Singida, Hamisi Nguli na anayefuatia ni makamu meya manispaa ya Singida,
Hassan Shabani Mkata.
Na Nathaniel Limu, Singida
HALMASHAURI
ya Manispaa ya Singida inatarajia kutumia zaidi ya shilingi 350
milioni, kwa kujenga machinjio ya kisasa katika eneo la Ng’aida kijiji
cha Kisaki.
Hayo
yamesemwa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Joseph Mchina
wakati akitoa taarifa yake ya ujenzi huo mbele ya kikao cha baraza la
madiwani.
Amesema
eneo hilo lililoridhiwa kwa ujenzi huo na serikali ya kijiji cha
Kisaki,lina ukubwa wa ekari 6.72,na jumla ya zaidi ya shilingi 11.2
milioni, zimetengwa kwa ajili ya kulipa fidia kwa wakazi watakaohamishwa
kupisha ujenzi huo.
Akifafanua,Mchina
amesema manispaa imeibua maradi huo ikiwa ni kutekeleza mkakati wa
kuboresha mazao yatokanayo na mifugo hususani nyama na ngozi.
Aidha,,
Mkurugenzi huyo amesema kuwa machinjio ya awali ambayo yalianza
kujengwa eneo la Manguanjuki na ujenzi huo ukagharimu shilingi
52,650,000,umesitishwa kwa madai kwamba eneo hilo linafaa zaidi kwa
ujenzi wa hoteli ya kitalii.
“Uthamini
uliofanyika mwaka 2010/2011,ulionyesha kuwa thamani ya jengo hilo na
eneo lilipojengwa,ni shilingi 195 milioni.Menejimenti imependekeza kuwa
atafutwe mwekezaji wa kununua jengo hilo ili fedha
itakayopatikana,ichangie kwenye ujenzi wa machinjio ya kisasa
itakayojengwa katika eneo la Ng’aida”,amesema Mchina.
Mchina amesema mwekezaji atafutwe kwa njia ya kutoa matanagazo kwenye magazeti,radio,televisheni na mbao za matangazo.
No comments:
Post a Comment