Pages

KAPIPI TV

Saturday, March 1, 2014

CHADEMA WAZIDI KUCHANJA MBUGA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KALENGA


Mgombea kupokelewa Lumuli

Meneja wa Kampeni za mgombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Alphonce Mawazo na mgombea, GraceTendega, wakipokelewa na wakazi wa kijiji cha Lumili mkoani Iringa kwenye muendeleo wa kampeni za chama hicho.
Mawazo na akinamama
Meneja wa Kampeni za mgombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Alphonce Mawazo na mgombea, GraceTendega, wakizungumza na akinamama wa kijiji cha Lumuli, katika kikao maalumu baada ya mkutano wa kampeni, zilizofanyika kijijini hapo.
Mawazo kumbeba mtoto 1
Meneja wa Kampeni za mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Alphonce Mawazo akiwa amembeba mtoto Zakina Miwela anayesoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Lumuli, ambaye ni mtoto wa kiongozi wa CCM katika kijiji cha Lumuli, anavyoonekana masikini kutona na sare zake za shule kuchanika, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo.
Mawazo kumwelezea mtoto
Meneja wa Kampeni za mgombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Alphonce Mawazo, akimwelezea mtoto Zakina Miwela, anayesoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Lumuli, ambaye ni mtoto wa kiongozi wa CCM wa kijiji hicho, anavyoonekana bila viatu na sare zake kuchanika, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo.
Heche kuhiutubia Lumuli
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema taifa, John Heche, akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Lumuli, wakati wa kampeni za kumnadi mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga kupitia chama hicho, Grace Tendega uliofanyika kijijini hapo.

No comments: