Mjumbe
wa Bodi ya Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu nchini (Tanzania
Human Rights Defenders Coalition) Dkt. Hellen Kijo Bisimba akitoa neno
la ufunguzi wakati wa warsha ya siku moja iliyowakutanisha watetezi wa
Haki za Binadamu nchini na Jeshi la Polisi jijini Dar leo.
.Asema dunia nzima inajua mvunjifu wa kwanza wa haki za binadamu ni dola
.Polisi pia ni binadamu wanahitaji kutetewa na mitandao ya haki za binadamu nchini
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
MKOSAJI
na mvunjifu mkubwa wa haki za binadamu ni serikali kutokana na
mazingira halisi ya utendaji na mfumo mzima wa utawala katika serikali
nyingi duniani. Imeelezwa.
Akizungumza
kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki
za Binadamu nchini, Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC)
kwa wakuu na makamanda wa Jeshi la Polisi nchini, Jaji Mstaafu, Thomas
Mihayo amesema kwa mfumo wa utawala katika nchi nyingi duniani mkosaji
mkuu wa haki za binadamu ni serikali.
“dunia
nzima inajua kwamba serikali ndio mkosaji mkuu wa haki za binadamu na
maana halisi ya serikali ni dola na mahakama tu kwisha,” amesema Jaji
Mihayo
Jaji Mihayo amesema kuwa kwa hali ya kawaida dola ikimkamata mtu au
mhalifu lazima mpeleke katika mahakama ili sheria ichukue mkondo wake wa
kawaida.
Naibu
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Abdurahman Kaniki, akitoa hotuba
yake ya ufunguzi kwa niaba ya IGP Ernest Mangu, kwenye warsha ya siku
moja iliyowakutanisha viongozi waandamizi wa Jeshi hilo na watetezi wa
Haki za Binadamu nchini.
Kwa
upande wake, Mjumbe wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Dkt
Helen Kijo Bisimba akitoa neno la ufunguzi amesema warsha hiyo inatoa
fursa nzuri kwa watetezi wa haki za binadamu na Jeshi la Polisi
kuboresha kazi zao za utetezi wa haki za binadamu nchini.
Amesema
kwa ujumla haki za binadamu hazipewi bali ni haki ya msingi ambayo mtu
anazaliwa nayo ili zinaminywa aidha kupitia mtu kwa mtu au taasisi au
mfumo wa utawala.
“Kazi
za watetezi wa haki za binadamu na Jeshi la Polisi zinaendama na msingi
ni utetezi wa haki za binadamu pamoja na mali zao,” alisisitiza
Naye, Mratibu wa kitaifa wa Mtandao huo, Onesmo Olengurumwa akiwasilisha
mada yake ya (The Concept of Protection and Security Management for
Human Rights Defenders and Social Organization) amesema kuwa taaluma
inaweza kutumika kutetea haki za binadamu katika maeneo mengi hapa
duniani.
Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Polisi
nchini, umuhimu wa kushirikiana kati ya Jeshi hilo na Asasi za kutetea
Haki za Binadamu ili kuleta tija katika nyanja za kiuchumi, kijamii na
kisiasa.
Amesema
pia kupitia mada hiyo kwamba jamii inadhani kwamba anayepaswa kutetewa
ni mwananchi tu lakini pia hata polisi naye ni binadamu anapaswa kuwa na
mtetezi pale ambapo haki yake ya msingi inapovunjwa.
“Mpaka sasa Tanzania haina sheria yeyote inayomlinda mtetezi wa haki za
binadamu lakini tunaendelea na mchakato na ni matumaini yetu serikali
itaridhia kuwa na sheria hiyo hapa nyumbani,” alilisitiza
Naibu
Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini, Abdurahman Kaniki amesema
kuwa jeshi la polisi nchini litaendelea kuimarisha mahusiano kati ya
jeshi hilo na watetezi wa haki za binadamu nia ni kudumisha amani na
utulivu nchini.
Sehemu
ya makamishina na makamanda wa mikoa na maafisa waandamizi wa Jeshi la
Polisi nchini wakifuatilia mada mbalimbali kwenye warsha hiyo ya siku
moja jijini Dar es Salaam.
“majukumu ya jeshi la polisi na watetezi wa haki za binadamu nchini
yanafanana kwa kila hali ni kulinda na kutetea haki za wananchi na mali
zao,” amesema Naibu IGP Kaniki
Kamishina
Kaniki alilisitiza kwamba ni muhimu wadau wote kuzingatia sheria za
nchi, taratibu na kanuni katika kutafuta haki mbalimbali ili kudumisha
amani na utulivu nchini.
“nachukua
nafasi kuwakaribisha wadau wote wa haki za binadamu na makundi mengine
kushirikiana na jeshi la polisi katika kulinda na kutetea haki za
binadamu nchini,” alisisitiza
Kamanda
wa Polisi Arusha, RPC Liberatus Sabas amesema kwa muda mrefu watu wa
utetezi wa haki za binadamu na makundi mengine huwa wanasahau kwamba
polisi pia ni binadamu nao wanahitaji utetezi kutoka kwa watetezi hao wa
haki za binadamu.
Naibu
Inspekta General wa Jeshi la Polisi nchini, Abdurahman Kaniki
(kushoto), Mratibu wa THRDC Taifa, Onesmo Olengurumwa (katikati) pamoja
na Mkurugenzi wa Mafunzo na Oparesheni, Kamishina Paul Chagonja
wakifuatilia mbalimbali ilizokuwa ikitolewa na washiriki wa warsha hiyo.
Mratibu
wa THRDC Taifa, Onesmo Olengurumwa akiwasilisha mada yake juu ya Ulinzi
na utawala wa haki za binadamu kwa mashirika ya watetezi wa Haki za
Binadamu pamoja na Polisi.
Pichani juu ni Meza kuu na chini ni Baadhi ya Wakuu na Makamishina wa
Jeshi la Polisi nchini wakifurahia jambo wakati wa uwasilishwaji wa mada
mbalimbali kwenye warsha ya siku moja iliyowakutanisha viongozi
waandamizi wa Jeshi hilo na watetezi wa Haki za Binadamu nchini.
Kamishina
wa kanda maalum ya Dar es Salaam, RPC, Sulemain Kova akichangia mada
katika warsha ya siku moja kuhusu Haki za Binadamu na ushirikiano kati
ya Jeshi la Polisi na watetezi wa Haki za Binadamu nchini.
Kamanda
wa Polisi, Arusha Liberatus Sabas akizungumza umuhimu wa kujali pia
askari polisi kwa sababu na wao pia ni Binadamu wanahitaji utetezi
kutoka kwa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotetea Haki za Binadamu
nchini.
Kamanda
wa Polisi, Lindi, RPC Zeloithe Stephen akitoa nasaha kuhusu miiko na
kanuni za Jeshi la Polisi jinsi zinavyotetea na kulinda Haki za Binadamu
(Police General Order).
Picha ya pamoja kati ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini na mgeni rasmi Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi nchini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TGNP, Bi. Usu Malya (kulia) akiteta jambo na Kamishina wa
kanda maalum ya Dar es Salaam, RPC, Sulemain Kova baada ya kupiga picha
ya pamoja.
No comments:
Post a Comment