Pages

KAPIPI TV

Saturday, March 1, 2014

BRIGEDI YA FARU YAADHIMISHA MIAKA 40 KWA KUFANYA USAFI NA KUCHANGIA DAMU

Baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania Brigedi ya Faru wakifanya shughuli za usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40 ya Brigedi ya Faru tangu kuanzishwa kwake hapa nchini.
Brigedia Jenerali Mathew Sukambi akiwa  na makamanda wengine katika maadhimisho hayo ambapo alishiriki kikamilifu shughuli za maadhimisho ya miaka 40 ya Brigedi ya Faru, askari wa JWTZ walifanya usafi Soko kuu la mjini Tabora,Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete na Stendi mpya ya mabasi Tabora mjini pamoja na kuchangia damu kwenye Benki ya damu Salama kanda ya Magharibi.
Baadhi ya askari walifukua pia mifereji katika barabara za Soko kuu la mjini Tabora ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40 ya Brigedi ya Faru
Usafi pia ulifanywa na askari hao Stendi mpya ya mabasi Tabora mjini
Askari akionesha pia ukakamavu wakati akitembea na kuendelea kufanya usafi eneo la Stendi ya mabasi Tabora mjini.
Baadhi ya askari wakipima afya zao kwa ajili ya kutaka kuchangia damu zoezi lililofanyika katika kambi ya Jeshi ya Mirambo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40 ya Brigedi ya Faru.
Afisa wa benki ya damu kanda ya magharibi akizungumza na mmoja kati ya askari aliyetaka kupima afya yake
Askari wa JWTZ Brigedi ya Faru walichangia damu na kulifurahia zoezi hilo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 40 ya Brigedi ya Faru.




































No comments: