Meneja
wa NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki, akifungua kikao cha waratibu wa
mfuko wa Taifa Bima ya Afya na wale wa mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)
ambacho kilitumika kukumbushana juu ya utoaji huduma bora kwa
wananchama.Kulia ni afisa matekelezo na uratibu NHIF mkoa wa
Singida,Isaya Shekifu na kushoto ni Edwin Mwangajilo afisa udhibiti
ubora NHIF.(Picha na Nathaniel Limu).
Afisa
matekelezo na uratibu wa mfuko wa taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa
Singida, Isaya Shekifu akitoa mada yake kwenye kikao cha wataribu wa
mfuko wa NHIF na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) mkoa wa Singida.Kikoa
hicho kililenga kubadilishana uzoefu juu ya utendaji kazi,ili kuboresha
zaidi huduma za mifuko hiyo.Kushoto ni meneja wa NHIF mkoa wa Singida,
Agnes Chaki.
Afisa
udhibiti ubora NHIF mkoa wa Singida, Edwin Mwangajilo,akitoa mada yake
kwenye kikao cha waratibu wa NHIF na CHF kilichofanyika kwenye ukumbi
mdogo wa mikutano wa kanisa katoliki mjini Singida.Kushoto ni meneja
NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki.
Baadhi
ya waratibu wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na wale wa mfuko wa Afya
ya Jamii mkoa wa Singida, waliohudhuria kikao cha kubadilishana uzoefu
katika utendaji kazi, ili kuboresha huduma zaidi.
Picha ya pamoja.
Na Nathaniel Limu, Singida
WARATIBU
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), na Mfuko wa Afya ya Jamii
(CHF) mkoani Singida,wamehimiza kuwa makini zaidi kukabiliana na wimbi
la madai ya kughushi, kwa madai kwamba vitendo hivyo,vitachangia
kudhoofisha huduma zinazotolewa na mifuko hiyo.
Wito
huo umetolewa na meneja wa NHIF mkoa wa Singida,Agnes Chaki,wakati
akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha waratibu wa NHIF na CHF mkoani
hapa, kilichofanyika kwenye ukumbi mdogo wa mikutano wa kanisa katoliki
mjini hapa.
Alisema
kuna baadhi ya watoa huduma si waaminifu na wanaleta madai ya kugushi,
na mfuko umejiandaa kikamilifu kuhakikisha unadhibiti vitendo hivi ili
kutimiza lengo la msingi la kuwapa huduma bora wanachama wake
“Ninyi
waratibu ninawaomba ndugu zangu, tusaidiane katika kupambana na hili
tatizo.Mnapokutana na watoa huduma,naomba mjaribu kuwaelimisha kuwa wawe
wanatibu kwa kuzingatia miongozo ya NHIF na ile ya wizara.Wahakikishe
kile wanachokitoa kinakuwa ni sawa na wanacho wasilisha NHIF….mfano
katika dawa”,alisema Chaki.
Aidha,meneja
huyo wa mkoa, alisema mwanachama,mratibu au kiongozi ye yote akisikia
au kuona kuna vitu/vitendo vinafanyika kinyume na taratibu za
NHIF,tafadhali atoe taarifa mapema ofisi za NHIF mkoani hapa,ili
ziwezekufuatiliwa mapema kabla havijaleta madhara kwa mfuko.
Kwa
upande wake afisa matelekezo na uratibu NHIF mkoa wa Singida,Isaya
Shekifu,akitoa mada yake ya majukumu ya waratibu wa NHIF/CHF,aliwataka
waratibu hao kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa uadilifu na kwa
ushirikiano baina yao ili kuongeza ufanisi na pia wanajitambulisha
kikamilifu katika vituo vyao vya kazi,ili wanachama wa mifuko
hiyo,waweze kuwafahamu na kuwatambua .
“Pia
hakikisheni mnatatua mapema matatizo/kero zinazohusu wanachma wa
NHIF/CHF pamoja na watoa huduma na muandae taarifa za utekelezaji kila
baada ya miezi mitatu”,alisema Shekifu.
Afisa
huyo wa maelekezo na uratibu,alisema NHIF inategemea endapo waratibu
watatimiza majibu wao kwa uhakika, malalamiko kuhusu huduma za NHIF
yatapungua na huduma zitaboreka.
Pia
afisa udhibiti na uhakiki ubora wa NHIF mkoa wa singida ,Dr.Edwin
Mwangajilo aliwasisitizia waratibu wa NHIF kuhakikishia wanapitia madai
kwa uangalifu ili kuepusha makosa ambayo yanaweza kupunguza kiasi cha
malipo ya madai kwa watoa huduma.
“Tunategemea
mtafanya kazi zenu kwa ufanisi na uadilifu na kuhakikisha mnasimamia
vituo vyote vile vya serikali,binafsi na mashirika ya dini ili wanachama
wetu wa NHIF na CHF wapate huduma bora ,alifafanua Mwangajilo.
No comments:
Post a Comment