Pages

KAPIPI TV

Sunday, February 16, 2014

HATARI KUBWA "MAJAMBAZI YAVAMIA KWA BUNDUKI KILA SIKU ZAIDI YA MADUKA MATATU TABORA MJINI"

Katika hali isiyokuwa ya kawaida hapa Tabora mjini kwa maeneo mbalimbali limeibuka wimbi la ujambazi wa kutumia silaha na kupora kwenye maduka ya vitu mbalimbali yakiwemo ya vibanda vya M-pesa na Airtel Money ambapo majambazi kati ya watatu hadi wanne wamekuwa wakifanya unyama huo wastani wa maduka mawili hadi matano kwa usiku mmoja.

Vyanzo vya mtandao huu vimeeleza kuwa majambazi hao ambao kwasasa wamekuwa kero kwa wafanyabiashara wamekuwa wakivamia maduka kuanzia majira ya saa mbili na nusu usiku hadi saa tano huku wakidaiwa kutumia silaha bunduki pamoja na mapanga.

Kwa mujibu wa maelezo ya vyanzo hivyo wastani wa kati ya shilingi laki sita hadi shilingi elfu kumi zimekuwa zikiporwa na majambazi hao ambao hadi sasa pamoja na kuwa wanatumia silaha hizo lakini hakuna raia aliyeripotiwa kuuawa kutokana na vitendo vya uharifu wa majambazi hayo.

Hata hivyo askari wa Jeshi la Polisi ambao wameimarisha ulinzi mkali kila eneo la mjini Tabora lakini jambo la kushangaza majambazi hayo ambayo yanadaiwa kuwa hayaonekani kutumia vyombo vya usafiri pindi wanapofika kuvamia kwenye maduka na yamekuwa yakiendeleza  uovu huo kila kona ya mjini.

Tayari hadi sasa matukio kadhaa ya uporaji unaofanywa na majambazi hayo umekwisha ripotiwa kituo kikubwa cha Polisi Tabora.

No comments: