Pages

KAPIPI TV

Tuesday, October 22, 2013

KAMATI YA MAADILI TAIFA YA CCM YADAIWA KUWAPIGA STOP WANAOKISAIDIA CCM TABORA MJINI.

Habari muhimu kutoka ndani ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tabora mjini,imebainika kuwa baadhi ya wanaCCM wanaokisadia chama hicho katika utekelezaji wa Ilani yake wamepigwa marufuku kuendelea na shughuli za kukiimarisha chama hicho ambacho kilianza kupoteza mvuto kwa wananchi.

Moja kati ya mambo yaliyosababisha CCM hapa Tabora mjini kupoteza umaarufu wake linatokana na ukweli kwamba baadhi ya vigogo wa Chama hicho wanashindwa kutekeleza ahadi walizozitoa wakati wakiomba kura kwa wananchi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 jambo ambalo wananchi wanakitazama chama hicho kama ni moja ya mhimili inayoshindwa kuwasimamia watu wake.

Hata hivyo baada ya baadhi ya wanachama na makada kuliona hilo wakalazimika kupitia jumuiya mbalimbali kuanza mikutano  ya kuwafuaata wananchi huko waliko ili waweze kutambua kero na mahitaji yao hatua ambayo ilikwenda mbali zaidi hata kusababisha wananchi kurejesha imani na matumaini kwa  chama hicho na kuona kuwa kumbe wapo watu wakiamua chama kinaweza kuendelea kuwa na nguvu mbele ya umma uliokatishwa tamaa.

Licha ya kuwepo kwa juhudi hizo za kukiimarisha chama zinazofanywa na makada hao wa CCM  lakini kumekuwa na mtazamo hasi kwa baadhi ya vigogo na kuona kuwa huenda juhudi hizo zikawa ni sehemu ya kupokonya nafasi zao wakati uchaguzi mkuu utakapo wadia.

Hofu ikatanda kwa baadhi ya vigogo na kuamua kupeleka malalamiko kwa kamati ya maadili na hivyo hatua zikachukuliwa kuanzia sasa kwa kuwasimamisha wale wote wenye nia ya kuendelea kukisaidia chama hicho ambacho kwasasa tunaweza kutamka rasmi kimeingia kwenye wimbi la kudidimia kisiasa.

Aidha CCM wilaya ya Tabora kwasasa imemeguka kutokana na hali hiyo na hivyo kusababisha vyama vya upinzani kuanza kujiimarisha tena kwa kufanya mikutano inayoelezea migongano inayojitokeza ndani ya CCM.

Hivi sasa CCM Tabora mjini haifanyi mikutano ya hadhara wakati vyama vya upinzani hasa Chadema kikiendelea kuvuna idadi kubwa ya wanachama wapya.

"Tunauhakika hata ikitokea sasa hivi uchaguzi mkuu CCM tunaimwaga vibaya maana tayari viongozi wao hawana jipya zaidi ya kuelekeza fikra zao kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 huku wakitelekeza kero za wananchi na baya zaidi ni hiyo vita ya ndani kwa ndani ndio inawasumbua"alisema mmoja kati ya viongozi wa vyama vya upinzani.  

 

No comments: