Mtoto Seif Salumu(4)ambaye ametekwa tangu tarehe 1 oktoba 2013 hadi sasa bado hajapatikana huku mtekaji akiweka masharti ya kupatiwa kiasi cha shilingi laki tano kwa njia ya M-PESA kwa nambari 0769 119061 ili aweze kumwachia huru. Mtoto huyu ambaye alikuwa akiishi na mama yake mzazi hapa manispaa ya Tabora alitekwa wakati akitokea shule ya awali ambako alikokuwa akisoma huko katika msikiti wa Kanyenye.Juhudi za kumsaka mtoto huyu ziligonga mwamba pale mtekaji alipoleta kiatu kimoja kwa njia za siri alichokuwa amevaa mtoto huyu akiambatanisha na barua ikitaka apatiwe pesa hiyo haraka. |
No comments:
Post a Comment