Pages

KAPIPI TV

Friday, September 6, 2013

WANANCHI-"YAANI JAMANI BUNGENI SASA HIVI...UNAWEZA HATA KUACHWA UCHI!"

bungeletu_42678.jpg
Mbunge wa Mbeya mjini mh. Sugu akitolewa nje na askari wa bunge mjini Dodoma bila hata kujali utu na heshima yake na pengine haki za kibinadamu....Kufuatia tukio hilo baadhi ya wananchi wamekuwa na maoni tofauti ambapo wapo ambao wamefikia kuchoshwa na hayo yanayotendeka Bungeni ambako kimsingi ndio sehemu pekee inayoandaa na kutengeza mustkabali wa maisha ya watanzania lakini imekuwa vinginevyo mbali na vitendo vya matusi na kejeli lakini pia imeshuhudia ngumi na kudhalilishana.

WANANCHI:- "Hivi ustaarabu uko wapi?...Je ni kweli kwamba naibu spika alishindwa namna ya kutatua hilo lililotokea au ndio kusema matumizi ya aina ipi ya kutumia kiti hicho alichopewa dhamana na wananchi?.....Au yanayotokea ni kwasababu ya kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi?...AMA KWELI CHELEWA KUFA UTAYAONA YA ULIMWENGU YALIVYO,...KURA ZETU SASA ZINATUMIKA VIBAYA SIO SIRI,...HALI HII INAFANYIKA KWA WABUNGE, JE KWA SISI WANANCHI WA KAWAIDA?  

No comments: