Pages

KAPIPI TV

Thursday, September 5, 2013

HATIMAYE MTOTO AKATWA MKONO MMOJA WA KUSHOTO,WAKULIA NAO HATARINI

Hatimaye mtoto Hamisi Rajabu(13)mkazi wa Isevya manispaa ya Tabora ambaye alipigwa shoti ya umeme kwenye Transfoma iliyoko Shule ya msingi Bomba mzinga wakati alipokuwa akicheza eneo jirani,amekatwa mkono mmoja(kushoto)kati ya mikono yake miwili iliyokuwa imeathiriwa vibaya na umeme huo mkali.Hata hivyo mtoto huyo ambaye alilazwa katika hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete bila kupatiwa matibabu ya kueleweka,alianza kuoza mkono huo wa kushoto baada ya kupewa ruhusa ya kurudi nyumbani kabla ya kurejeshwa tena hospitalini hapo ambapo sasa amekatwa mkono huo.

No comments: