Pages

KAPIPI TV

Friday, September 6, 2013

"BARUA YA WAZI KWA MBUNGE WA TABORA MJINI"-MWANANCHI


BARUA NZITO na YA WAZI KWA MBUNGE WANGU

Mhe Ismail Aden Rage
Mbungewa Tabora mjini
S.L.P 42236
DAR ES SALAAM

YAH: MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2015

Kwako Mbunge

Somo tajwa hapo juu lahusika, awali ya yote nitumie fursa hii adhimu kwa niaba ya wakaazi wenzangu wa Jimbo la Tabora mjini kukupongeza kwa juhudi na jitihada zako unazoendeleza bungeni kwa ajili ya kutuwakilisha wananchi wako, hua tunakuona TBC, Akhsante sana!!

Nimeamua kukutumia barua hii ili iwe kama mchango wangu kwako ifikapo muda wa uchaguzi maana kuna watu huku wamekikania kiti chao ila usiogope sana kwani hii mbinu nayotaka kukupa hivi punde si mpya kihiivo, ila ilashawahi kutumiwa na mbunge flani hivi wa hapo Kigoma,

Mpango uko hivi, inabidi sasa na wewe uwatumie wasanii wa Muziki wazalendo wa Tabora kama ilivyokua kwa jirani yako, na wala usikhofu wapo wengi tu mie takutajia wachache tu, kuna Q CHIEF, EBBY SKILLZ, INSPECTOR HAROUN, PICO mzee wa kikongwe, BUFF G wa East Coast, SHILOLE, J.I mtoto wa Nzega, NK, kisha walipie fedha watoe NGOMA kali kupitia kwa Producer SHEDDY CLEAVER!!

Baada ya hapo tutaitengenezea video kali itakayonesha madhari na hali ya Tabora, Tutaonesha kilimo kilichotukuka cha TUMBAKU, ASALI, MATOBHOLWA, nk,

Katika Video hiyo nasi tuoneshe maeneo yetu mashuhuri kama vile MNARANI, MILAMBO SECONDARY, TABORA BOYS, TOWN SCHOOL, KIPALAPALA, ila mitaa mikongwe kama ule wa pale kwenu RUFITA tusioneshe maana unazidi tu kuchakaa labda uoneshe tu ule mgahawa uliokua unauza chai wewe kabla hujawa alwatan maana wakati mwingine Historia ni muhimu,, pia sishauri kuonesha SOKO KUU, HOSPITALI YA KITETE, wla bwawa la IGOMBE Linalo supply maji mjini kwetu na AIBU!!

Katika video ya wimbo huo tuwahusishe na watu mashuhuri Tanzania watokao Tabora kama kina Mhe Sitta, Mhe Kapuya, Mhe Lipumba, wasanii kama kina YUSUPH MLELA, DUDE, MAMAA NYAWANA, MAULID KITENGE, pia sio mbaya kama utapata picha za kina marehem Power chuma, Said mwamba kizota,, Dr Kigwangala, Adam Gosho, nk Hakyamungu utapata kura!!

Pia uweke japo ka clip kamoja tu jinsi unavyokuaga busy kule kwenye club yetu ya Simba maana kuna wajinga wachache huku wanadhani huko Dsm Umekaa tu bila ya kazi maalum japo hili litawaudhi watani wetu wa jadi YANGA, Utapata kura mpaka utashangaa!!!

Ila tu usijisahau ukaweka picha za kiwanda cha nyuzi maana hiyo sasa italeta tafrani si unaona jinsi kilivyochoka na kuchakaa!! ila tu uwakazanie hao wasanii wasasahau kusifia vijiwe vya kahawa na mwishooni kabisa uweke japo picha mbili tu za barabara mbovu za kutokea Nzega HAKYAMUNGU UTATUSUA mHeshimiwa!!!

Ni mimi Kijana wako mtiifu
Mwingizi Maundu

No comments: