Pages

KAPIPI TV

Wednesday, September 18, 2013

"ACHENI TUIMARISHE CHAMA CHETU,MANENO MANENO YA NINI?-MWAKASAKA

Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tabora mjini Bw.Emmanuel Mwakasaka akipeana mkono na mmoja wa Chipukizi kata ya Ntalikwa manispaa ya Tabora baada ya kumkabidhi Kadi ya uanachama  wapya wa Chipukizi Tabora,wakati wa ziara rasmi ya kukijenga CCM kupitia jumuiya ya UVCCM Wilaya ya Tabora mjini. 
Mmoja kati ya viongozi wa UVCCM Wilaya ya Tabora mjini Bi.Rosemary Cloud akionesha furaha yake katika ziara hiyo ya UVCCM kata ya Ntalikwa ambayo imeonesha mafanikio makubwa kwa kuongeza idadi wa wanachama wa CCM kupitia jumuiya hiyo ya Vijana.
Katika ziara hii Mjumbe wa kamati kuu ya CCM wilaya ya Tabora Bw.Mwakasaka mbali ya kukabidhi Jezi za mpira wa miguu,alikabidhi pia fedha zaidi ya shilingi Mil.moja kusaidia shughuli za miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata hiyo ya Ntalikwa.
 Na Mwandishi wetu Tabora.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tabora mjini Bw.Emmanuel Mwakasaka amewataka wanachama wa CCM wakiwemo viongozi kuelekeza nguvu zao katika kukijenga chama hicho badala ya kuendekeza majungu na manung'uniko yasiyo na msingi.

Bw.Mwakasaka ameyasema hayo katika kata ya Ntalikwa manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kukiimarisha CCM iliyoandaliwa na Jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM wilaya ya Tabora.

Katika ziara hiyo Mwakasaka alifikia kutoa tamko hilo baada ya kuwepo kwa baadhi ya kauli za wanaccm kutafsiri vibaya malengo ya  ziara hizo ambazo zinafanyika mara kwa mara wakidai kuwa ni kampeni za maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

"Jamani acheni tukijenge chama,...tusingoje wakati wa uchaguzi tu ndio tuanze kuwa karibu na wananchi hii sio nzuri kwetu,...na mnaoona kuwa ni kampeni jueni kuwa tunapoteza muda wenzetu wa vyama vya upinzani wanafanya sana mikutano karibu kila siku"alisema Mwakasaka.

Sambamba na hilo Bw.Mwakasaka alisisitiza kuwa ni vema tukaendelea kukijenga chama chetu hatua ambayo itatusaidia kukabiliana na vyama vya upinzani kwa sisi kupata ushindi mkubwa wakati wa uchaguzi utakapowadia.

Aidha CCM kupitia Jumuiya ya UVCCM wilaya ya Tabora hivi sasa kimekuwa kikifanya mikutano ya mara kwa mara hatua ambayo inadaiwa kuwa inazidi kukiimarisha Chama hicho na kurejesha imani kwa wananchi wilaya ya Tabora.  


No comments: