MBUNGE wa jimbo la
Sikonge,mkoani Tabora,Said Nkumba amelinyooshea kidole jeshi la polisi wilayani
humo kwa madai limekuwa likiwambikizia kesi wananchi.
Alitoa kauli hiyo hivi karibuni
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya CCM wilayani humo.
Nkumba alisema asingependa
kugombana na watendaji wa serikali ama vyombo vya ulinzi na usalama ama polisi
kwani kero ambazo zmekuwa akipokea kama mbunge
toka kwa wananchi ni malalamiko ya kubambikwa kesi na polisi.
“Wapo polisi ambao si
waaminifu na wamekuwa wakijihusisha na matendo ya rushwa,kubambika wananchi
kesi na mara nyingine wamekuwa hawatoi dhamana kituoni hadi watuhumiwa watoe
kitu kidogo.”alisema Nkumba.
Alisema ifikie mahali
wananchi washirikiane na polisi kwenye ulinzi shrikishi lakini sasa hivi
wananchi wanaishi kwa uadui na baadhi ya askari polisi hapa Sikonge.
Alisema pamoja na malalamiko
hayo bado vijana wenye kufanya kazi ya bodaboda nao wamekuwa wakilalamikia sana matendo ya askari
polisi ama trafiki kuomba rushwa bila kufanya makosa yoyote.
Katika hatua nyingine mbunge
huyo aliliomba jeshi la Sungusungu lipewe elimu kuhusiana majukumu yao kwani mara kadhaa
wamekuwa wakikengeuka namna ya kufanya kazi zao na kukuta wakivunja sheria.
Baadhi ya wananchi waliozungumza
na mtandao huu walisema wamefikia mahali sasa watakuwa wakichukua sheria
mkononi kwani wahalifu wakikamatwa wamekuwa wakiachiwa polisi na kuja uraiani
kuwatishia.
“Tumechoshwa sana na hali hii
tutachukua maamuzi yetu…..hata huo ulinzi shirikishi kwa sasa hatutaki
tumechoshwa.
Kamanda wa jeshi la polisi
mkoani Tabora Peter Ouma alisema hana taarifa hizo lakini wapo wananchi ambao
wanakuwa si wakweli.
“Hivi mfano wananchi wanapiga
kura ya kutuhumu mtu kuwa jambazi hapo kabambikwa kesi…..waje kwake walete
ushahidi wa kubabikizwa kesi hizo atashughulikia mara moja.” Alisema.
No comments:
Post a Comment