Bw.Salumu Msamazi diwani wa Kata ya Ikomwa Manispaa ya Tabora. |
Nashukuru madiwani wenzangu pamoja na viongozi wa CCM kwa nafasi zao,wameweza kunipigania hata kufikia hatua ya kushinda katika uchaguzi huu wa kumpata mgombea mmoja kutoka ndani ya chama chetu atakaye wania nafasi hii adhimu ya Unaibu Meya wa halmashauri ya manispaa ya Tabora.
Licha ya kuwa kulikuwa na makambi ambayo yalitupeleka kubaya
lakini wadau wangu walikuwa
imara kuhakikisha hawawezi
kubadili msimamo wao juu yangu na kuhakikisha
wananiweka katika nafasi
hii kwa kunipigia
kura zipatazo 19 dhidi
ya mpinzani wangu wa
karibu Bw.Waziri Mlenda
ambaye alikuwa akitetea
nafasi hiyo aliyoitumikia
kwa mwaka
mmoja huku akiambulia
kura 14.
Hii imenifanya nijisikie
kuwa nina deni kubwa
mbele ya madiwani
wa halmashauri ya
manispaa ya Tabora
na wananchi
wao kwa ujumla.
NINASEMA KWA KAULI
MOJA NITAKUWA NAIBU MEYA WA
WANANCHI NA SIO MPIMA VIWANJA NA
KUSABABISHA MIGOGORO YA ARDHI,…..”IMEFIKIA
HATUA MHESHIMIWA DIWANI
ANAKUWA MPIMA VIWANJA
JAMBO HILI NI WAPI NA WAPI”…KWA
MAANA HIYO HATA
DIWANI UNAJIKUTA UNAKOSA NAFASI YA
KUWATETEA VIZURI WANANCHI
WALIOKUCHAGUA UNAKUWA BIZE
NA WAPIMA VIWANJA WENZAKO.....Akacheka kidogo akiashiria kufurahia ushindi wake.
Hivi ndivyo nilivyo
msikiliza Bw.Salumu Msamazi
muda mfupi tu mara
baada ya kuchaguliwa
kukiwakilisha chama kuwania
nafasi ya Unaibu Meya wa manispaa
ya Tabora.
Bw.Msamazi
ambaye katika siku chache
hizi za mchakato
wa kumpata naibu Meya
amekumbana na changamoto
kadhaa hata za
vitisho dhidi ya
maisha yake lakini hakuvunjika moyo
kwani alitambua kuwa
kila jambo la
heri haliji kwa
lelemama bali lazima
liwe ni la mapambano
aidha kufa au
kupona.
Si hivyo tu
bali alitambua kuwa
katika mapambano hayo
pia Sapoti anayopewa na
washiriika wake ikisimamiwa kwa uweza
mkubwa wa Mwenyezimungu
ndio nguzo yake
kuu katika ushindi
dhidi dhahma zote
alizoundiwa kwa wakati
huo wote, kipindi
alichokiita kigumu sana hata
akaifikiria pia familia yake
akaona JAMII AU
WANANCHI NI BORA
ZAIDI NA HIVYO KUPATA
NGUVU YA KUENDELEA
NA MTANANGE HUO WA
HATARI LAKINI SALAMA.
‘’NITASHIRIKIANA NA MADIWANI
WENZANGU NA NITAKUWA
NA MSIMAMO KUTEKELEZA
MAAMUZI YA VIKAO
BADALA YA MAAMUZI
BINAFSI KAMA ALIVYOKUWA
AKIFANYA ALIYEMALIZA MUDA WAKE”Alisema
Msamazi.
HABARI ZILIZOKWEPO MITAANI.
Vita hiyo aliyokuwa akipigwa
Bw.Msamazi imeelezwa kuwa
ilikuwa ikihusisha hata viongozi wakubwa wa
CCM Mkoa na
baadhi ya Wabunge jambo
ambalo lilidhihirisha kuwa
makundi ni kitu
kibaya kabisa ndani
ya CCM na
tena ni hatari
kuliko inavyofikiriwa sasa.
Eti inasemekana kuwa kuna baadhi ya
wagombea katika kinyang’anyiro hicho waligushi hata
vyeti vya elimu
zao,……Mhmm,..Kwa hili mie tena
simo nawaachia wanaCCM
wenyewe ambao ndio
walikuwa wakizagaza hayo
ingawa kuna baadhi
ya vyeti niliviona
kwa macho yangu
lakini Mhmm,…NISIJE NIKANG’OLEWA
MENO NA KUCHA
KWA KUTUMIA PRIZE
KWANI BADO NI
MWANDISHI MCHANGA SANA
KATIKA FANI HII
YA KUWAJUZA WATU.
No comments:
Post a Comment