Pages

KAPIPI TV

Tuesday, August 13, 2013

CHINA KUJENGA MJI WA KISASA TABORA,NEEMA YANUKIA,WAWEKEZAJI WENGI WAJA KUWEKEZA.

Balozi wa China nchini Tanzania Bw.Lu Youqing akiwa na mwenyeji wake mkuu wa mkoa wa Tabora  wakati wakipata maelezo ya eneo la kujenga Bandari ya nchi kavu huko Inala nje kidogo ya mji wa Tabora.
Barabara ya Tabora - Itigi kwa kiwango cha Lami ambapo balozi Lu alitembelea. 

NIONAVYO MIMI
Ama kwa hakika Mungu si Athumani,amini usiamini kuna kila dalili kwa mkoa wa Tabora kuwa sehemu inayovutia kwa utafutaji wa maisha.

Pamoja na kuwa tulizoea kusema kuwa Tabora hakuna kitu,Tabora pakavu sana,Tabora hakuna lolote,Tabora majungu tu,Tabora wachawi,Tabora mauaji ya kupindukia na mambo kadha wa kadha  ...Lakini hayo  yote hivi karibuni katika kipindi kifupi kijacho huenda  yakabaki kuwa historia tu ikiringanishwa na jitihada zinazofanywa na Serikali ya mkoa wa Tabora katika kutafuta wawekezaji.

Si vibaya hata kuliona hilo kubwa lililofanywa na Rais Kikwete la kuweka barabara za kiwango cha Lami ikiwa ni mkakati wa kuufungua mkoa wa Tabora  ambapo kwa wengine wamekuwa wakibeza jitihada hizo na kuletea maneno mengi yasiyo na mashiko kila upande,Lakini  hili sasa wenzetu wa Serikali ya mkoa wa Tabora wakalitazama tofauti kidogo kwa maana ya kuona mbali zaidi. 

Wakafumbua macho yao na kuona baada ya barabara za lami nini maandalizi yetu kama mkoa,...bila kufanya ajizi wakaanza mpango mkubwa wa kutafuta wawekezaji kila kona ili mradi tu kuona kama kweli mabadiliko yatakuwepo au la kama walivyozoea wenyeji ambao wengi wao hawataki mabadiliko na kubaki na msemo "eti Tabora ilishalaaniwa na waarabu haiwezi kupata maendeleo"jambo ambalo ni fikra mfu kwa ulimwengu wa sasa wa Sayansi na Teknolojia.

Hapa nakubaliana na vichwa vilivyokaa  na kutafakari namna ya kuwaondoa wakazi wa Tabora pale walipo na kujaribu kuwafikisha eneo ambalo nao wataona kuwa ni nafasi yao kipekee katika kuyaona maisha katika mwanga bora,kumbe MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA INAWEZEKANA.

Hongereni sana  Jamani kwa kuumiza vichwa hili lilikuwa gumu sana kulifikia hapa Tabora.

Wawekezaji kutoka china  imeelezwa kuwa tayari wamethibitisha wapo tayari kuwekeza kwa kununua tumbaku ambayo katika kipindi hiki chote wakulima wamekuwa wakinyonywa na makampuni ya wazungu ambayo yamekuwa yakinunua zao hilo kwa kadri wanavyotaka wao tena naweza kusema kuwa kwa dhuruma kubwa wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa vyama vya msingi ambao nao kwa sehemu kubwa huchangia kuzidisha umasikini kwa wakulima wenzao.  

Tukiachana na zao la tumbaku ambalo ndilo zao kuu la biashara na linaloingiza pato kubwa lisilo mnufaisha mkulima,fursa nyingi zilizotangazwa ambazo zitaleta mabadiliko makubwa  Tabora,Uwekezaji katika maeneo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa bandari ya nchi kavu,mji wa kisasa wa china,ujenzi wa Stand mpya ya kisasa utakaotokana na kukamilika kwa barabara hizi za kiwango cha Lami na ukizingatia Tabora kama vile ipo katikati hivi!!...Kwa maana  kila itakuwa vigumu kwa wafanyabiashara wakubwa kuendesha shughuli zao pasipo kuifikiria Tabora ambayo sasa itakuwa kiunganishi kikubwa hata na nchi za Rwanda,Burundi,Uganda na pengine hata Kongo pia.

Sasa  naomba nitoe tahadhari kwa wananchi wenzangu wa Tabora,...Jamani msibweteke maana ninaloliona kwenu kwasasa ni kubaki walalamikaji pale wenzetu kutoka mikoa jirani watakapo kuja na kuchangamkia fursa mbalimbali hizi zinazoanza kunukia.....Jamani msije ,mkawalaumu viongozi wa serikali kwani hata mbeleko waliyojaribu kutubebea hadi sasa itakatika na matokeo yake tutadondoka chini na kuumia,...Lamsingi tuchangamkie fursa hizi zinakuja.

Balozi wa China nchini Tanzania Bw.Lu Youqing ametembelea mkoa wetu wa Tabora hii ina maanisha ni jitihada za Serikali ya mkoa  ndio zimefikia hatua hiyo na niwazi kwamba Balozi pia amefuatana na Jopo la viongozi wa Asasi za Wawekezaji huko China ambapo wameonesha kuridhishwa na fursa zilizopo Tabora na kukubali kuwekeza katika nyanja mbalimbali.



     

  



No comments: