Pages

KAPIPI TV

Friday, August 16, 2013

ASKARI 'FEKI' NI AIBU KWA JESHI LA POLISI NCHINI?


Na Esther Macha wa matukiodaima.comMbeya
 
KWA tukio hili jeshi la polisi limetia aibu kubwa hakuna budi kwa jeshi hilo kufanya uchunguzi wa kina kubaini askari wengine bandia ambao wapo katika  Mikoa mbali mbali .

Ninachoweza kusema kuhusu askari huyu feki wa kikosi cha usalama barabarani  ni kwamba kazi hiyo amekuwa akiifanya kazi hiyo  kwa muda mrefu tena kwa ujasiri mkubwa lakini ujasiri huo nadhani ulitokana na kupata nguvu kutoka sehemu fulani .

Lakini kama  kweli jeshi la polisi likifanya uchunguzi wake kwa kina yawezekana likaweza kuwabaini askari wengine wa kikosi cha usalama barabarani ambao ni feki bila jeshi hilo kufahamu kinachoendelea kwenye vituo vya polisi .

Ili kuweza kubaini hilo jeshi la polisi nchini kupitia kikosi chake cha usalama barabarani lifanye kazi yake ya kuchunguza askari mmoja baada ya mwingine kwa kuanzia kuangalia vyeti vyake halisi na majina wanayotumia, pamoja na vyeti vya kuzaliwa  kama  ni halisi.

Kwani yawezekana hata askari waliopo kazini si askari halisi kwa utambuzi wa veti vyao hivyo jeshi la polisi lifanye kazi hii kwa umakini ili kubaini vyeti feki kwa askari wake.

Kwa kusema hili naweza kusema kuwa askari huyu licha ya kufanya kazi hiyo kwa muda mrefu bila jeshi hilo kufahamu lakini bado aliweza kufanya kazi hiyo kwa kujiamini tena kwa kufuata taratibu zote za kazi za usalama barabarani kana kwamba amepata amesomea  kazi hiyo.

Binafsi ninachoweza kusema ni kwamba tukio hili kwa ujumla limeitia aibu jeshi la polisi kwani ni kitu ambacho hakiwezekani trafiki huyu bandia afanye kazi kwa muda wote huo bila kujulikana na uongozi na hata uongozi wa juu wa jeshi hilo.

Lakini pia kinachonishangaza ni kwamba askari huyu feki  mwenye  cheo cha sajini alidiriki hata kuwapangia kazi askari wadogo walio chini chake na hata askari hao wadogo wanaposhindwa kuwadhibiti madereva watukutu askari hao wadogo huwapeleka kwa askari huyo feki kwa lengo la kupigwa faini kutokana na kuogopwa  na madereva kwa ujasiri wake wa kazi.

Nioanavyo kuhusu hili ni kwamba kwa masuala ya kujeshi, hilo siyo kosa la mhusika ni kosa la polisi wenyewe kutokuwa makini katika utendaji wao wa kazi.

Kitakachoweza kushangaza umma ni pale askari huyu feki  kosa lake likipelelezwa kwa kasi na baadaye utasikia mara ooh kesi sijui imefanyeje  na mwisho huishia hivyo hivyo bila wananchi kujua hatima ya huyu askari bandia .

Mimi binafsi ninachoweza kushauri ni kwamba kama jeshi la polisi linahitaji kujisafisha hakuna budi kwa muhusika kuchukuliwa hatua kali na hata kama kulikuwa na watu Fulani ndani ya jeshi hilo ambao walikuwa  nyuma  yake kwa lengo la kumlinda wachukuliwe hatua.

Kwani askari huyu feki asingeweza kuifanya kazi hii kwa ujasiri bila ya kupata ujasiri toka kwa watu, kinachotakiwa ufanyike uchunguzi wa kina kwa askari huyu feki kwa utaratibu nae ataweza kuongea ukweli wake halisi jinsi gani aliweza kuifanya kazi hiyo na aliyempa ujasiri huo ni nani.

Askari feki kama hawa  wapo wengi sana hasa mikoani  na njia  zilizojificha wakiendelea na kazi kama kawaida kana kwamba ni sheria kwao kufanya kazi hiyo na hata waliofukuzwa kazi kazi katikas jeshi hilo kwa makosa mbali mbali pia wamo katika idadi hiyo yta askari feki .

Ili kuona  jeshi hilo linaondokana aibu hiyo pia lijaribu kuangalia hata askari wake ambao walifukuzwa kazi kwa makosa mbali mbali ndani ya jeshi hilo  ,kwani nao wanaweza kuwa sababu ya kulichafua jeshi hilo.

Kitu kingine ambacho naweza kusema ni kuhusu hawa askari kanzu wa jeshi la polisi waliopo katika mikoa mbali mbali nchini ,hawa nao jeshi la polisi inabidi lifanye kazi yake ya kiuchunguzi kubaini nao kama ni askari halisi  maana hawa nao wamekuwa wakichanganya wananchi .

Nadhani kuanzia sasa uongozi wa juu wa jeshi hilo uwe na utaratibu maalum kwa askari wake  hasa wa kikosi cha usalama barabarani na askari kanzu kuwa na vitambulisho maalum kwani yawezekana hata kitengo hiki cha askari kanzu pia kikawa na watu wa namna hiyo bila jeshi la polisi kufahamu.

Nionavyo kuhusu hili si jambo la kupuuza kwa ngazi za juu za jeshi la polisi  ili kuweza kunusuru jeshi hilo katika kashfa mbaya na hata kurudisha imani kwa wananchi ambao wamekuwa wakiamini kazi kubwa ya jeshi hilo.

Tukio la askari huyu bandia mwenye cheo cha sajini, (jina halikupatikana) alikamatwa na Polisi akiwa 'kazini' maeneo ya Tabata Kinyerezi akiwa amevaa sare mpya ya Askari wa Usalama Barabarani, akiwa na kikoti cha kuakisi mwanga na kofia nyeupe.
Pia trafiki huyo alikuwa na jalada pamoja na kitabu cha kutoza faini (Notification) kwa madereva wanaopatikana na makosa ya kukiuka sheria za usalama barabarani.

Katika taarifa ya gazeti hili la majira lilishuhudia trafiki huyo feki akiwa amekamatwa na Polisi na kisha kufikishwa Kituo Kikuu cha Polisi Kati, huku akijifanya amepoteza fahamu.
Ushauri wangu kwa jeshi la polisi wajiangalie vizuri katika utendaji wao wa kazi kwani wananchi wanazidi kukosa imani na utendaji wa kazi  wa jeshi hilo ,kitendo cha mpaka raia kuvaa sare za jeshi hilo kwa muda mrefu bila hata jeshi hili kutambua kitu gani kinaendelea ni aibu kubwa kwa jeshi.

Kama jeshi la polisi wanatakiwa kuanza kujiangalia upya na kujitafakari kwa haya matendo mabaya yaliyopo mbele yao na kujisafisha mbele  ya wananchi ambao wanawaongoza.

No comments: