Pages

KAPIPI TV

Friday, August 16, 2013

MTANZANIA MWINGINE AKAMATWA HONG KONG NA DAWA ZA KULEVYA AINA YA HEROIN.


kulevya 7432d
Kweli sasa Tanzania tunastahili Tunzo, tunaanza kujulikana kimataifa
Abiria wa Tanzania akamatwa Hong Kong na heroin ikiwa ndani ya mashine.

Kwa mara nyingine, maafisa wa Hong Kong katika kiwanja cha ndege wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya zilizokuwa zinasafirishwa kutokea Tanzania safari hii zikiwa zimefichwa katikati ya chuma cha mashine.
kulevya1 9e687
Dawa hizo aina ya heroin zilikamatwa katika nyakati mbili tofauti kwa jumla zikiwa na kilo 1.5 na thamani ya dola milioni 1.3 za Marekani.

Maafisa hao wanasema kwa kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu nyendo za wauza dawa na mbinu za kuficha dawa hizo, walilazimika kukikata chuma cha mashine hiyo ili kuziona.

Adhabu ya kupatikana na dawa za kulevya huko Hong Kong ni faini ya dola milioni 5 za Kimarekani.
Taarifa hii  imechapishwa kwenye tovuti ya Serikali ya nchi hiyo.

No comments: