Maamuzi dhidi ya kesi inayowakabili viongozi na wananchama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA yaliyokuwa yatolewe leo yatatolewa bila wao kuwepo yamepangwa jumatatu ujayo Augast 05.
Uamzi huo umetolewa na Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Tabora Simon Lukelelwa kufuatia kuchelewa kufika kwa washitakiwa wa kesi hiyo waliohifadhiwa gereza la Uyui mjini hapa.
Wakati maamuzi hayo yanatolewa na Jaji Lukelelwa washitakiwa wote watano wa kesi hiyo Henry John Kileo, Evodius Justian, Oscar Kaijage, Seif Kabuta n Rajab Kihawa hawakuwa katika chumba cha
mahakama majira ya saa tatu na nusu asubuhi.
Hii ni mara ya kwanza kuonekana mahakamani kuu ya Tabora kwa kesi nzito kama hii washitakiwa kucheleweshwa kufikishwa mahakamani kukabili tuhuma hata mashitaka yanayowakabili.
Washitakiwa walifikishwa mahakamni hapo majira ya saa nne na dakika arobaini na waliarifiwa na wakili msomi mwakilishi Emanuel Msyani kuwa shauri limepangwa tarehe tano mwezi ujao wakiwa ndani ya chumba cha madabusu ya mahakama.
Hii ni changamoto kwa serikali na vyombo vyake vya ulinzi na usalama dhidi ya wananchi wanaoishi wakiwa chini ya uangalizi kuhakikisha kuwa wanapohitajika wafikishwe mahala hapo kwa wakati na siyo walalamikiwe.
Kesi hiyo ya rufaa ya jinai namba 53/2012 ilifunguliwa na wakili wa utetezi Peter Kibatala na kuanza kusikilizwa julai 22/2013 mbele ya Jaji Lukelelwa ikoomba miongozo ya kisheria ikiwemo yaliyotolewa na
mahakama za wilaya na mkoa.
Shauri la maombi ya marejeo liliwakilishwa na wakili peter Kibatala anayewatetea washitakiwa akiiomba mahakama kuu ipitie majalada ya kesi mbili dhidi ya wateja wake zilizofunguliwa mahakama hizo baada
ya kuona maamuzi yake hayakutenda haki.
Wakili Kibatala alibainisha katika maombi hayo kwamba kutokana na maamuzi hayo ya mahakama za chini yameathiri pia haki za waomba rufaa ikiwemo ni pamoja na kuwanyima haki ya kupata dhamana.
Kwa upande wake serikali ilishindwa kujibu maombi hayo na badala yake ilijenga hoja kwamba walicelew kupata nyaraka hizo kwani walizipokea tarehe siku moja kabla ya kutajwa shauri hilo hivyo walishinda
kuzijibu.
No comments:
Post a Comment