Pages

KAPIPI TV

Saturday, August 3, 2013

TAKUKURU YAWANING`INIZA 12 MAHAKAMANI SIKONGE

.

Na Mwandishi,Sikonge

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU),wilayani  Sikonge
mkoa wa Tabora,imesema hadi kufikia mwezi julai 31,mwaka huu
imewafikisha watu 12 mahakamani kwa tuhuma mbalimbali zinazowakabili.

Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Sikonge,Manyama Tungaraza,alisema hayo
kwenye kikao cha baraza la madiwani wilayani humo.

Tungaraza alisema jumla ya kesi tano zimefunguliwa katika mahakama ya wilaya ya Tabora mjini.

Alisema baadhi ya kesi hizo ni vyama vya msingi vya ushirika kesi 3,kilimo (PADEP)kesi 3,ujenzi kesi 2.

Alisema kesi nyingine ni jeshi la polisi kesi 1,mipango kesi 1,elimu
kesi 1 na VEO vijiji kesi 1.



Alisema kesi hizo zimekuwepo hasa kutokana na malalamiko ambayo
yamekuwa yakipokelewa na ofisi yake kutoka kwa wananchi na kufanyiwa
kazi.

Tungaraza alisema licha ya kuwepo kwa kesi hizo baada ya kupata
malalamiko toka kwa wananchi bado wameendelea na zoezi la kutoa elimu
kwa wananchi,taasisi na wanasiasa hasa baraza la madiwani kila mara.

Hata hivyo Tungaraza aliwakumbusha madiwani hao jukumu la mapambano ya
rushwa ni la viongozi wote,madiwani na watendaji wa vijiji,vitongoji
kata na kwamba kila mtu atomize wajibu wake.

Aidha licha ya taarifa hiyo,kamanda huyo alitoa mada kwa
watendaji,madiwani na wageni waalikwa akikumbusha majukumu ya
TAKUKURU,kushauri na kuchunguza shughuli za taratibu za jamii,taasisi
za umma,sekta na binafsi.

Kamanda huyo aliongeza kuwa TAKUKURU pia imekuwa ikishauri na
kuchunguza taratibu za jamii,umma,na sekta binafsi ili kuwezesha
kugundua vitendo vya rushwa,ikiwemo usambazaji wa taarifa kuhusu
athari za vitendo vya rushwa kwa umma.

No comments: