MAMLAKA
ya chakula na dawa nchini (TFDA), kanda ya magharibi na
kati,imeteketeza bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu, zenye
thamani ya sh milioni 3.2.
Zoezi
la kuteketeza bidhaa hizo lilifanyika mkoani Tabora baada ya kufanyika
ukaguzi maalumu kwa wiki mbili kwenye maduka,majengo,Phamacy bohari ya
dawa na maeneo mengine muhimu.
Akizungumza
na waandishi wa habari eneo la kuteketeza bidhaa hizo,mkaguzi kanda ya
kati na magharibi,Abel Deule,alisema ukaguzi huo ulihusisha watalaam
toka ofisi ya mganga mkuu wa mkoa wa Tabora na halmashauri ya manispaa
Tabora na ukaguzi huo ulihusisha biashara ya chakula,dawa,vipodozi na
vifaa tiba.
Deule
aliongeza jumla ya majengo 192 yalikaguliwa na ambapo lengo lake ni
kuangalia majengo hayo,usafi,hali ya usajili na vibali toka mamlaka ya
chakula na dawa,(TFDA),hali ya ubora wa bidhaa za chakula,dawa,vipodozi,
vifaa tibauwepo vifaa bandia zenye viwango duni na uwepo vipodozi
vyenye viambata vyenye sumu.
Aidha
Deule alisisitiza kutokana na ukaguzi huo,licha wafanyabiashara hao
kuwa na uelewa,bado wamekuwa wakiuza vipodozi vyenye viambata vyenye
sumu vilivyozuiliwa kuuzwa na ktumika nchini kwa mujibu wa kifungu namba
88 (a) cha sheria ya chakula, dawa na vipodozi namba 1 ya mwaka 2003.
Alisema
bidhaa zilizokamatwa na kuteketezwa ni bidhaa za chakula tani 0.129 ya
thamani ya sh 775,000,bidhaa za vipodozi zilizoisha muda wa matumizi na
zenye viambato vyenye sumu tani 0.245 vya thamani y ash sh milioni
2,298,400 na dawa za binadamu tani 0.001 zenye thamani ya sh 158,000.
Aidha
aliongeza kwenye ukaguzi huo pia kulikutwa maziwa ya watoto ,Lactogen
namba 1 na 2 na NAN ambayo ni bandia, dawa ya chanjo ya mifugo ya
Newcastle (1-2) iliyositishwa kuuzwa,dawa bandia aina ya Doxycycline
Capsules gramu 100,pombe kali iitwayo Shujaa gin ambayo haijapata
usajili toka mamlaka ya chakula na dawa.
“Kutokana
na hali hiyo tumechukua hatua za maduka yaliyokutwa na vipodozi vyenye
viambata vya sumu….. wamiliki walilipa ada ya vibalivya
kuteketeza,wateja ambao majengo ambayo hayajapata usajiliwalijaza fomu
na kulipia ada kwa vibali husika ikiwemo duka moja kufungwa kutokana na
mmiliki kuwa mkaidi kwa maafisa.” alisema Deule.
Aliongeza
hata hivyo wakati wa ukaguzi wafanyabiashara walielimishwa kuhusu
bidhaaza vyakula,dawa.vipodozi,ikijumuishwa bidhaa za vipodozi zenye
viambato vyenye sumu,na bidhaa duni na bandia ya chakula (Lactogen 1/2
na NAN 1/2.
No comments:
Post a Comment