Hii ndio familia ya Mzee Machiya Luponyapumba mkazi wa kijiji cha Bulenya huko Igunga,familia hii kwasasa ipo hatarini kukosa makazi baada ya Mzee Machiya kuingia katika mkataba wa kukopa fedha kiasi cha Shilingi mil.10 ili baada ya miezi 6 alipe Shilingi mil.24,hatua ambayo Mzee Machiya amefanikiwa kulipa Shilingi Mil.15 lakini cha kushangaza mdai wake ambaye amefahamika kwa jina la Wangu Joseph amemfungulia kesi ya madai ya Shilingi Mil.24 na hivyo anatakiwa kulipa haraka iwezekanavyo na tayari Mahakama ya wilaya ya Igunga imekamata mali zake ikiwa ni pamoja na gari aina ya Hino Coasta na ifikapo tarehe 2 April 2013 nyumba yake ambayo wanaishi familia ya watu 85 itauzwa kwa mnada na tayari Dalali amekwisha bandika matangazo katika nyumba hiyo.
Sakata hili sasa likafungua ukurasa mpya wa kufikishana mahakamani ambako Mzee Machiya alitakiwa kulipa kiasi cha shilingi Mil.10 licha ya kupunguza deni kama alivyofanya na kibaya zaidi Mzee Machiya aliwekwa ndani mara mbili huku mahakama ikimtaka amlipe mdai wake.
"Mimi sijakataa kulipa lakini sio hiyo pesa ninayotakiwa kulipa kwani tayari nilishatoa Mil.15,jamani naomba watu wa msaada wa sheria mnisaidie,ina maana sisi tusiojua kusoma haki zetu zinapotea tu?...hayo ni maswali ambayo amekuwa akilalamikia Mzee Machiya kutafuta msaada ingawa kwasasa ukibahatika kukutana naye njiani ameonekana kujisemea mwenyewe kana kwamba anataka kupata ugonjwa wa akili.
Imeelezwa kuwa sababu kubwa ya Mzee Machiya kuingia mkataba wa mkopo huo mbali na kutojua kusoma na kuandika lakini alitaka fedha hizo ziweze kumsaidia kumtibia mke wake ambaye kwasasa ni marehemu.
Katika mkataba ambao alivutika kuingia Mzee Machiya na Bw.Wangu Joseph walitiliana saini majira ya saa kumi na mbili jioni katika ofisi ya hakimu wa mahakama ya Ziba wilayani Igunga huku ikiwekwa dhamana ya gari aina ya Noah,hekari 200 za shamba,Gari ndogo 2 aina ya Mark II na Ng'ombe wapatao 20.
Aidha kwa upande mwingine katika makubaliano ya mkataba huo wa kupatiwa kiasi cha shilingi Mil.10,Mzee Machiya aliwekewa masharti ya kutozwa shilingi lakini tano kama endapo angekuwa tayari kuahirisha kuingia mkataba huo uliogubikwa na wimbi la Mizengwe.
Mzee Machiya ambaye inafahamika kuwa hajui kusoma wala kuandika alikubali kwa shingo upande kupokea shilingi Mil.8 huku akiahidiwa Mil.2 kwa siku iliyofuata.
Wakati ulipowadia wa kurejesha shilingi Mil.24,Mzee Machia inadaiwa kuwa alijikongoja na kulipa kiasi cha shilingi Mil.10 na pia kumruhusu mdai wake Joseph aiuze gari aina ya Noah aliyoiweka kama dhamana ya mkopo ambayo pia inasemekana iliuzwa kwa mizengwe kiasi cha shilingi Mil.5.
"Mimi sijakataa kulipa lakini sio hiyo pesa ninayotakiwa kulipa kwani tayari nilishatoa Mil.15,jamani naomba watu wa msaada wa sheria mnisaidie,ina maana sisi tusiojua kusoma haki zetu zinapotea tu?...hayo ni maswali ambayo amekuwa akilalamikia Mzee Machiya kutafuta msaada ingawa kwasasa ukibahatika kukutana naye njiani ameonekana kujisemea mwenyewe kana kwamba anataka kupata ugonjwa wa akili.
No comments:
Post a Comment