mwili wa kijana Paul Raphael Mtekele ukiwa umefunikwa baada ya kuteketezwa kwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kuiba pampu ya kupulizia dawa mazao ya shilingi 25,000 katika kitongoji cha Tosamaganga B wilaya ya Iringa vijijini usiku wa leo (Tunaomba radhi kwa picha hizi)
WANANCHI wanaosadfikika kuwa na
hasira kali wakazi wa njiapanda ya Tosamanganga wilaya ya Iringa
vijijini mkoani Iringa wamemuua kwa kichapo mtuhumiwa wa wizi kijijini
hapo Paul Raphael Mtekele na mwili wake kuuchoma moto baada ya
kijana huyo kuvamia nyumba zaidi ya mbili kijijini hapo na kuiba
mali mbali mbali ikiwemo pampu ya kunyunyuzia dawa mazao yenye
thamani ya Tsh 25,000
Tukio hilo la kinyama limetokea
majira ya saa 9 usiku wa kuamkia leo katika kitongoji cha Kipanga B
katika kijiji cha Njiapanda ya Tosamanganga wilaya ya Iringa
vijijini jimbo la Kalenga .
Wakizungumza na mtandao huu wa
www.francisgodwin.blogspot.com leo eneo la tukio wananchi wa eneo
hilo akiwemo Juma Mwakawago ambae pia katibu wa huduma za jamii
kijiji hicho cha Tosamaganga amesema kuwa katika kijiji hicho
kumekuwepo na matukio mbali mbali ya uharifu na watu kuibiwa mali na
wanaodaiwa kufanya hivyo ni pamoja na marehemu huyo na kundi lake.
Hata
hivyo kijana huyo kabla ya kuuwawa alikiri kujihusisha na matukio
mbali mbali ya wizi kijijini hapo pamoja na kuwachomea nyumba wakazi wa
eneo hilo na maeneo mengine pale wanapokosa kupata mali walizozifuata
kwa ajili ya kuiba .
Pia alidai lengo lao kwa siku ya jana ni kwenda kuiba eneo la Ilula katika moja kati ya maduka ya mji huo wa Ilula ila wenzake waliopanga nao walichelewa kumfuata na hivyo yeye kuamua kufanya shughuli hiyo kijijini hapo na kuomba kusamehewa .
Alisema kuwa mbali ya matukio mbali
mbali ya uharifu kujitokeza katika kijiji hicho ila usiku wa jana
nyumba mbili za wakazi wa kitongoji cha Kipanga B zilivamiwa na
wezi hao na kuporwa mali na kupelekea wananchi kufanya msako
uliopelekea kumkamata kijana huyo akiwa katika harakati za kuvunja
mlango wa nyumba ya mkazi mmoja wa kijiji hicho na baada ya kubanwa
ndipo alipokwenda kuonyesha pampu hiyo iliyoibwa usiku huo.
Hata hivyo alisema kuwa baada ya
kipigo kikali kijana huyo ambae sasa ni marehemu alilazimika kutoa
orodha ndefu ya vijana ambao wamekuwa wakishirikiana katika uharifu
,orodha ambayo imehifadhiwa na wakati wowote kijiji kitaendesha
msako wa kukamata mmoja baada ya mwingine.
Mmoja kati ya wazazi katika eneo
hilo Delophina Mtavilalo ambae pia ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Iringa vijijini alisema kuwa vitendo vya wizi katika kijiji
hicho vimezidi na kuwa mbali ya wizi bado wanawake wamekuwa
wakibakwa na kupokonywa mali zao .
Hivyo alisema tukio la kijana huyo
kuuwawa mbali ya kuwa linasikitisha ila bado linapaswa kuchukuliwa
tahadhari kubwa kwa vijana wanaoendelea kufanya shughuli za wizi na
kuwataka vijana kuachana na shughuli hizo na badala yake kujiunga
katika vikundi vya kiuchumi .
Mwenyekiti huyo wa CCM wilaya
aliwataka pia wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa
kuwaua watuhumiwa wa uharifu na badala yake mara baada ya kuwakamata
wahakikishe wanawafikisha mbele ya vyombo vya sheria kwa hatua zaidi
badala ya kuwaua kinyama kama hivyo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo
mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Njia panda ya Tosamaganga
Dominic Ndenga alisema kuwa kijana huyo alikuwemo katika orodha ya
vijana wanaojihusisha na vitendo vya wizi katika kijiji hicho.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa tayari
kijiji kimefikisha taarifa kwa mkuu wa polisi wilaya ya Iringa
(OCD) kumjulisha juu ya vitendo vya wizi katika kijiji hicho pamoja na
unywaji wa pombe kupita kiasi ambapo wananchi wamekuwa wakishinda
katika pombe usiku kuja na kuwa kuanzia sasa dawa yao inachemka .
Pia alisema orodha ya majina ya
wizi iliyotajwa na marehemu huyo itafanyiwa kazi mara moja ili
kuhakikisha mtandao wa uharifu katika kijiji hicho unakomeshwa na
kuahidi kufufua ulinzi wa kijadi ( sungusungu )
Baba wa kijana aliyeuwawa mzee
Raphael Mtekele alisema kuwa kijana wake alikuwa akituhumiwa kuhusika
na vitendo vya wizi mara kwa mara na kupelekea kuhama kijijini hapo
na kuhamia eneo la Ipogolo katika Manispaa ya Iringa na kuwa ni juzi
tu ndipo aliporejea kijijini hapo na usiku wa leo kuuwawa .
No comments:
Post a Comment