WADAIWA KUUA MTOTO WAO KWA KUMTUMBUKIZA MAJINI KWA MADAI KUWA HAFANANI
NA BABA YAKE,
Na Anthony Mayunga-Serengeti.
Januari 4,2013.
KUTOKUAMINA kwa wanandoa wawili wakazi wa kitongoji cha Mahanga kijiji
cha Gusuhi kata ya Nyambureti wilayani Serengeti kumepelekea kuua
mtoto wao wa miaka 2 kwa kumtumbukiza Mto Tirina ,kwa madai kuwa
mtoto huyo hafanani na baba yake.
Tukio hilo ambalo linadaiwa kuibua hasira kwa jamii linadaiwa kutokea
januari 1,muda usiojulikana mwaka huu ,kijijini hapo,limethibitishwa
na uongozi wa kijij,kata na polisi wilayani hapa.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho Marwa Nyahende amewataja watuhumiwa hao
kuwa ni Matiko Msamba(25)na Mkami Msamba (18) lakini jina la mtoto
aliyekufa halijajulikana.
Akisimulia mkasa huo mmoja wa mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la
Simba mkazi wa kijijini hapo alisema kuwa maiti ya mtoto huyo
iliokotwa eneo la Mahaga wilayani Bunda na kuanza ufuatiliaji .
“Polisi wa kituo kidogo cha Mugeta wilayani Bunda walipopata taarifa
hiyo walifuatilia ,wakidhani kuna watu wamechukuliwa na mto wakati
wanavuka….na taarifa zikatufikia tukaanza ufauatiliaji”alisema.
Alisema kuwa maiti hiyo ilibidi izikwe kando kando ya mto huo januari
2 ,lakini watuhumiwa hawakuweza kushiriki hali iliyoibua hisia kutoka
kwa jamii kwa kuwa mtoto wao alikuwa haonekani.
“Majilani walilazimika kuuliza kwa kuwa waliwaona siku ya tukio wakiwa
na mtoto wao lakini sasa haonekani na hawakushiriki hata mazishi…huyo
mama akasema walikwenda kumwachisha kwa wazazi wake eneo la Kemgongo
Nyamatoke…katika ufuatiliaji ikabainika hakuna mtoto huko ,ndipo kazi
ikaanzia hapo”alisema.
Naye mkazi mwingine alisema kuwa walimweka chini ya ulinzi mama huyo
huku mme wake akitokomea porini na alipopigwa na wananchi akasema kuwa
wao waliamua kumtumbukiza majini afe kwa kuwa mme wake hakuwa na imani
na mtoto huyo.
“Mme wake alisema ili ndoa idumu inabidi waue mtoto huyo kwa kuwa
hawafanani naye kwa upendo aliokuwa nao kwa mme wake akakubali wamuue
kwa kumtumbukiza majini ili waishi kwa raha kama mme na
mke”alibainisha.
Maelezo ya mama huyo yaliibua hasira kwa wananchi wakitaka
wamshambulie hata kumuua ,lakini busara ikatumika na kumweka chini ya
uangalizi wa mwenyekiti wa kitongoji na ndugu zake wakajitokeza na
kusaidiana kumpeleka kituo cha polisi Kenyana kwa usalama wake.
Diwani wa kata hiyo Nicholaus Maro alipoulizwa alisema kuwa tukio hilo
alikiri kutokea na kudai ni la kwanza katika eneo hilo na ambalo si
kawaida na linatakiwa kukemewa na hatua kali kuchukuliwa dhidi ya
wahusika.
Walikokutana.
Inasemekana watuhumiwa hao walikutana katika kijiji cha Mosongo kama
wapenzi na baadae kuchukuana kama wanandoa wakahamia kijijini hapo na
mtoto huyo akazaliwa ,hata hivyo waliishi kwa kutoaminiana huku mme
akidai mke wake alimsaliti na kupata mimba nje ya ndoa yao.
Polisi wanaendelea na uchunguzi ikiwa ni pamoja na kumsaka mtuhumiwa
Msamba ambapo waliomba wananchi wasaidiane ili kuhakikisha anakamatwa
na kufikishwa mbele ya sheria.
Hivi karibuni mama mmoja mkazi wa kijiji cha Kwitete wilayani hapa
ameua mwanae wa miaka 3 kwa kumpiga,kisha kumchoma kwa chuma kwa madai
kuwa alikula kipande cha nyama na kuchezea kinyesi baada ya
kujisaidia.
Mwisho.
AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUUA MTOTO WAKE.
Na Anthony Mayunga--Serengeti
Januari 4,2013.
MWANAMKE aliyekamtwa kwa tuhuma ya kosa la kuua mwanae kwa kumpiga
kisha kumchoma kwa choma kwa kosa la kuchezea kinyesi na kula mboga
amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Serengeti
kujibu shitaka linalo mkabili.
Aliyefikishwa mbele ya mlinzi wa amani Judith Semkiwa ni Ghati Range
(30) mkazi wa kijiji cha Kwitete kata ya Kyambahi wilayani hapa.
Akisomewa shitaka hilo mbele ya mlinzi wa amani ,Judith Semkiwa wa
mahakama ya Mwanzo Mugumu ,mwendesha mashitaka inspekta msaidizi wa
polisi,Alfred Marimi alidai tukio hilo limetokea desemba 30 majira ya
saan 3:00 usiku mwaka jana eneo la nyumbani kwa mshitakiwa katika
kijiji cha Kwitete kata ya Kyambahi wilayani hapa.
Alidai kuwa Ghati Range alimpiga mtoto wake Ryoba Juma Nyandama
(3)sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia fimbo kisha kumchoma kwa
chuma cha moto sehemu za kichwani na mikononi baada ya mtoto huyo
kujisaidia haja kubwa na kuanza kuchezea kinyesi na pia kula mboga
chunguni.
Mwendesha mashitaka huyo alidai baada ya mwanamke huyo kumoa adhabu
hiyo mwanae ,alimfungia ndani ya nyumba kwa wiki nzima bila kumpeleka
hospitali hali iliyopelekea mtoto huyo kupoteza maisha.
Mshitakiwa hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo
wa kisheria kusikiliza kesi hiyo ya mauaji,amerudishwa mahabusu hadi
januari 16 mwaka huu itakapotajwa tena.

No comments:
Post a Comment